Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Umoja
wa Vijana wa CCM (UVCCM) umesema matamshi
yaliotamkwa na Mbunge wa Singida Mashariki(Chadema)Tundu Lisu ni ya
kusaka umaarufu wa kisiasa hatimae awanie urais akiwawacha solemba
Edward Lowassa na mshirika wake Fredrick Sumaye .
Aidha
Umoja huo umesema povu linalowatoka viongozi wa upinzani akiwemo Lisu,
ni kielelezo cha kutapatatapa na kufiisika kisiasa kufuatia utendaji
unaokubalika wa serikali ya Rais john Magufuli huku wakiwa wakionekana
kuvunjika matumaini na kukata tamaa.
Hayo
yametamkwa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka wakati
alipozumguza na viongozi, wanavyuo na wanachama wa CCM katika ukumbi wa
CCM kizota mjini kigoma mkoani hapa.
Shaka
alisema maneno ya Lisu hayawezi kuitingisha serikali ya CCM na kwamba
serikali inayomnanga iwapo itamtaka akamatwe kwa kuvunja sheria za
nchi, vyombo vya dola havitasita kumuweka kizuizini .
Alisema
kuna kila ishara ya mwanasiasa huyo wa upinzani inayoonyesha
akiyatamani maisha ya gerezani baada ya kuchoshwa na yale ya uraiani
ambapo sasa ameamua kutamka upuuzi , kujeli na upumbavu kinyume na
ustaarabu.
"Tumemtafakari
na kubaini ana nia ya kuwania urais mwaka 2020, anachotaka ni kuwaacha
kwenye mataa jamaa zake kina Lowasa na sumaye, ila ajue akizidi kueneza
matamshi ya kipuuzi anaweza kukamatwa na kutupwa mahali"Alieleza shaka
Alisema
hakutawakuwa hakuna maana ikiwa mtu mmoja anainanga Serilali na kuipaka
matope, kumkejeli Rais akiyewekea kisheria na kikatiba na wananchi
wkaendelea kutazamwa macho.
"Lisu
si kama papai ambalo kama litaweka ndani litaooza na kuharibika,
anaweza kukaa huko kwa usalama wake na wa nchi,tuneruhusiwa kisheria
kufanya siasa za vyama vingi kwa ustaarabu na uungwana na si kufanyiana
kejeli na dhihaka "Alieleza
Alisema
hata wakati wabutawala wa Baba wa Taiafa mwalimunjulius nyerere
walikywepo baadhi ya wanasiasa waliotaka kuidharau serikali,walikamatwa
kwa usalama wao na kufichwa mahali kwa muda fulani.
"Lisu
ni nani mbele ya mamlaka za kisheria na kikatiba, tunadhani anatatapata
nyingi nasaba hivyo ajiandae siku yoyote anaweza kukutwa na msiba,msiba
wa kujitakia hauna pole, dola yoyote haifanani na kitambaa cha deki"
Alisisitiza.
Uvccm ina
ushahidi wa kutosha toka kwa watu wa karibu na Lisu wamemwambia kwamba
ndiye snayetosha kuwania urais ndani ya chadema mwaka 2020 hivyo
ametakiwa atafute "kick'ya kisiasa ili kuvuruga Sumaye na Lowassa .
Hata
hivyo shaka alisema si kosa kwa Lisu kuwania urais ila anachotakiwa ni
kujipima kibusara na kibusara, kiuwezo na kiupeo kama ni mtu
anayestahili na sahihi ambaye anayetosha kuomba nafasi hiyo au la .
Vile
vile uvccm umewataka watanzania kumpuuza mwanasiasa huyo wa chadema kwa
kadri atakavyotamka kwasababu mtu yoyote mwenye ufahamu na uelewa
hawezi kuyadhijaki mamlaka ya Rais na nafasi alionayo.
"Ujasiri
wa kuidhihaki mamlaka ya Rais ni sawa na mtu juha aubounguani
anayejaribu kutupa jiwe katikati ya mzinga wa nyuki au mpumbavu kuncgeea
simba sharubu "Alieleza shaka.
Kaimu
huyo katibu mkuu aliwashukuru wazee wa mkoa wa kigoma kwa kumtawaza na
kuwa mwana kigoma huku akiwaahii hatawangusha ila malipo anayoyaanda
kuonyesha shukran na furaha yake ni kuongiza harakati za kisiasa
zitakazomuondoa zito Kabwe kwenye nafasi ya ubunge wa kigoma mjini mwaka
2020 .