KITENGA:MAONYESHO YA NANE NANE YAPO PALE PALE

Katibu Tawala akitoa maelezo juu ya maadhimisho ya siku ya nane nane kwa kanda ya Kaskazini.



Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,Richard  Kwitega amesema kuwa maonyesho ya wakulima maarufu kama nane nane ambayo yamekuwa yakifanyika katika viwanja wa Themi Njiro yataendelea kuwepo kama kawaida.

Ameyasema hayo baada yakutokea sitofahamu kwa wananchi kutokana na iliyokuwa taasisi yakusimamia maonyesho hayo (TASO) kuzuiliwa kuendelea kuratibu maonyesho hayo.

Aidha, amesema kwa mwaka huu maonyesho hayo yataratibiwa kwa ushirikiano baina ya Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Sekretarieti za Mikoa ya Arusha,Kilimanjaro na Manyara pamoja na TASO.

Hata hivyo ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha ikiwa ndio mwenyeji wa maonyesho hayo ndio imepewa jukumu lakusimamia uwandaaji wa shughuli zote katika viwanja hivyo.

Ametoa wito kwa washiriki wote wa maonyesho hayo kwa mwaka huu  2017 kuanza maandalizi mapema ikiwemo ulipaji wa ada ya ushiriki katika ofisi zilizokuwa za TASO ndani ya viwanja vya nane nane ambapo kwa sasa kuna maafisa walioteuliwa kutoka katika Wizara na Sekretarieti ya Mkoa kutumia ofisi hizo kwa shughuli hizo.

Pia shughuli nyingine za Maandalizi zikiwemo kuwasilisha mahitaji ya idadi ya waoneshaji, Magari, na taarifa nyingine zifanyike katika ofisi za TASO kabla ya Julai 20,2017.

Kwa mwaka huu maonyesho hayo yatabeba kauli mbiu isemayo “Zalisha kwa tija mazao na bidhaa za Kilimo,Mifugo na Uvuvi ili kufikia uchumi wa kati”,ambayo yataanza rasmi Agosti moja,2017 nakumalizika Agosti 10,2017.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post