'CASTLE LITE UNLOCKS' YASISITIZA WASHIRIKI KUJIANDIKISHA KWA WINGI KWA AJILI YA TAMASHA LA MUZIKI LINALISUBIRIWA KWA HAMU NCHINI


 Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Idara ya Kuunganisha Wateja Afrika Mashariki, George Kavishe (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu kuhamasisha washiriki kuhudhuria kwa wingi katika tamasha kubwa la muziki ambalo halijawahi kushuhudiwa Tanzania. Kutoka kushoto ni Mratibu wa Malipo wa kwa Tigo Pesa, Newton David na Meneja Masoko wa TBLKitengo cha Bia Laini Afrika Mashariki, Amou Majok.


Mratibu wa Malipo wa kwa Tigo Pesa, Newton David (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Ofisa Masoko kutoka Kampuni ya CFAO Motors Ltd, Angelina Ndege akizungumza katika mkutano huo kuhusu kudhamini tamasha hilo.
Meza kuu.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wasanii wa hapa nchini watakaotoa burudani katika tamasha hilo. Kutoka kulia ni Vanessa Mdee, Nareel Mkono na Aika Marreale.



Na Dotto Mwaibale

KAMPENI ya Castle lite unlocks inahamasisha washiriki kuhudhuria kwa wingi katika tamasha kubwa la muziki ambalo halijawahi kushuhudiwa Tanzania.

Wito huo umetolewa na Meneja wa mahusiano ya wateja wa kampuni ya Tanzania Brewaries Limited (TBL) kwa Afrika Mashariki, George kavishe katika taarika yake kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo, ambapo alitumia fursa kuwataja wadhamini na wabia wa kampeni hiyo. 

“Kwa mara nyingine tena tunawakumbusha wapenzi wa muziki, hasa walioko katika jiji la Dar es salaam na maeneo ya karibu kujiandikisha kwa wingi kwani tukio hilo la aina yake linakaribia” alisema Kavishe, akiongeza kuwa washiriki watapata fursa adimu sana ya kufurahia bonanza lamuziki litakalo tayarishwa na brand ya kipekee ya bia, Castle Lite hivi karibuni.

Akitangaza washirika, kavishe alipongeza mchango wao, akisema kwamba wametekeleza jukumu kubwa katika mafanikio ambayo kampeni hiyo imefikia mpaka sasa.

Alitaja wadhamini kama vile Tigo Tanzania (mshirika  rasmi wa mawasiliano ya Simu), Clauds FM (Mshirika kama chombo cha habari), CFAO Motors  (Mshirika katika usafirishaji), Marlborona Serena Hotel Dar es Salaam (Mshirika katika malazi).

“Tunawashukuru sana washirika wetu kwa kukamilisha juhudi zetu katika kuelekea kwenye tamasha la nne la muzikiambalo linahakika kuwa litakuwa ni chanzo cha mabadiliko makubwa katika tasnia ya muziki wa wandani”, Kavishe amesema kuhusu Bonanza kubwa ambalo limepangwa kufanyika tarehe 22 mwezihuu wa julai katika ukumbi wa Leader’s Club hapa Dar es salaam. 

Kwa mujibu wa Kavishe, kampeni ya Castle Lite Unlocks ni harakati kubwa ambapo bia ya Castle  Lite  imekuwa  inabadilisha  mwelekeo  wa  mchezo  kwa  kuleta wasanii wakubwa na mashuhuri wa imataifa kuja kufurahia pwani za Afrika kwa kutoa burudani ya kipekee ya ‘Extra Cold’ katika tamasha kubwa la‘Castle Lite Unlocks’

“Tamasha la mwaka huu litakuwa na neema ya kutembelewa na wanamuziki maarufu na wakongwe wa Hip Hop, huku wanaochipukia wakiwa wanasindikizwa na wanamuziki maarufu wanaotikisa bongo flava Tanzania wakiongozwana Diamond Platnumz” alisema Kavishe, akiwataja wasanii wengine watakao kuwepo kuwa ni, Casper Nyovest Kutoka Afrika kusini, Vanessa Mdee, kundi la Weusi  na Navy Kenzo ambao ni wa hapa hapa nchini Tanzania.

Kavishe alishauri wapenzi wamuziki kununua tiketi kupitia Tigo Pesa namba 0674 444 444 na kwenda kuzichukua katika Tigo Shop yoyote hapa Dar es salaam. Mitandao  mingine ya simuinaweza kununua tiketi kwa kuchagua “mitandaomingine” katika menyu ya simu pesa zao na kununua kwa kupitia namba hiyo hiyo ya malipo. 

“Manunuzi ya tiketiyanaenda kwa kasi sana kwa hiyo ni na wasisitiza watu wote kununua tiketi zao sasa kwa sababu hii ni tukio ambalo haupaswi kukosa. Castle Lite ni bidhaa bora ambayo inakuletea uzoefu wa hali ya juu. 

Watu wategemee burudani ambayo haijawahi kutokea hapa Tanzania, tumeandaa tamasha hili kwa hali ya juu, kiwango cha usalamani cha hali ya juu na mpangilio wakipekee wa ukumbi wa tamasha ambao utawaacha watu wakiwa katika hali ya mshangao” alisema Kavishe.

“Gharama ya tiketi ni Tshs 20,000 akini  watejawatakaol ipa kwa Tigo  Pesa watafurahia punguzo la bei la Tshs 5,000, hivyo watalipa Tshs 15,000 kwatiketi moja,” alisema Kavishe, huku akiongeza kwamba wateja wataweza kujipatia tiketi zao kutoka katika maduka ya huduma kwa wateja ya Tigo (Tigo shop) yaliyopo karibu nao. 

Alizitaja sehemu ambalko wanaweza kwenda kuchukua tiketi zao kuwa ni pamoja na: Mlimani City-Mlimani City Mall, Makumbusho (mkabala na), Palm Beach Residence-Ocean Road, Nkurumah- Nyerere Road- Gold Star, Buguruni-Rozana, Quality Center-Quality Center Mall, JM Wall- Hotel Harbor View, Masaki- Haille Selassie Road, Kariakoo-Msimabazi/Pemba Street, Manzese Darajani, Kigamboni-Ferry, Tegeta-Kibo Complex na Mbagala- Oil Com Gas Station.

Kwa upande mwingine, Kavishe aliongeza kwamba wateja pia wanaweza kupata tiketi kwa pesa taslimu Sh 20,000/= katika maeneo yafuatayo, Clouds Fm-Mikocheni, Funzone Shamo Tower-Mbezi Beach, Leader’s Club-Kinondoni na duka la Bron to Shine-Mwenge.
Kampeni ya Castle lite Unlocks itahudhuriwa na washindi 22 kutoka Zambia na 19 kutoka Tanzania ambao wamejishindia tiketi za “kiwango cha VIP” ambayo itawapatia fursa ya kusafirishwa kwa ndege mpaka Jijini Dar es salaam, kukaa katika hotel maarufu kwa siku mbili, kufurahia burudani ya hali ya juu, kupelekwa na kurudishwa kutoka katika tamasha wakati huo huo ukiwa unapokea huduma za VIP kwa wakati wote. 

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post