Mshindwe na mlegee kugombanisha wastaafu
Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Umoja
wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umewakanya wanasiasa
waliohamia upinzani toka CCM wanaoeneza maneno ya chuki na mifarakano
kwa lengo la kuwagombanisha marais wastaafu washindwe na walegee
kwasababu kila Rais mstaafu alitimiza haki na wajibu wake alipokuwa
madarakani.
Pia
Umoja huo umeelezea kukerwa kwake na tabia ya baadhi ya viongozi wa
upinzani ambao asubuhi hutamka maneno haya na jioni wanapojisahau,
hunena mengine bila ya kuwa na indhar wala kumbukumbu ya kutosha.
Onyo
hilo limetolewa jana katika kijiji cha Ubinza, wilayami Ubinza mkoani
hapa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka alipozungumza na
wanachamawa CCM na jumuiya zake katika ukumbi wa CCM akiwa katika
ziara yake ya kikazi ya siku tano Mkoani humu .
Shaka alisema wapo baadhi ya wanasiasa wa upinzani wengi wakiwa ni wale waliokihama Chana
Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na vyama vingine, wanajaribu kwa namna
moja au nyingine kuwafarakanisha marais wastaafu na Rais aliyeko
madarakani kwasababu zao binafsi na za kisiasa bila kupima menono yao
wala kutafakari kwa kina .
Aidha
Shaka akimzungumzia Rais wa awamu ya kwanza Baba wa Taifa marehemu
Mwalimu Julius Nyerere, alisema ameiachia heshima kubwa Tanzania katika
medani za kidiplomasia na kimataifa,akashirikiana na mwenzake Hayati
Sheikh Abeid Amani Karume hadi kuundwa Muugano wa Tanganyika na Zanzibar huku nchi yetu mahali popote uendapo duniani sasa ikitajika kwa wema na heshima ya juu.
Alisema
Awamu hiyo ya kwanza ya utawala wa Mwalimu Nyerere ndiyo ulioweka
misingi ya utaifa, kuwaungisha watanzania, kuhimiza matumizi ya lugha ya
Kiswahili kuwa ya Taifa, akajenga viwanda na kuanzisha kampuni za
serikali na mashirika ya umma pia akashiriki kizalendo katika harakati
za ukombzi Kusini mwa Afrika.
"Baba
wa Taifa Mwalimu Nyerere ndiye aliyetuunganisha na kutufanya tuwe
wamoja , amepigania uhuru, akaleta umoja wa kitaifa, amekomesha ukabila,
udini na ubaguzi wa rangi hadi kusimama kwa Taifa letu na kuwa moja "
Alisema Shaka.
Akiitaja
awamu ya Pili, alisema chini ya Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi
ndipo ilipofunguka milango ya biashara huria, kutolewa ruksa kwa kila
mmoja kujituma na kujitegemea kiuchumi ,kuanza ujio wa wawekezaji na
kutokea kwa fursa mbalimbali za kimaendeleo na kiuchumi.
Kaimu huyo Katibu
Mkuu aliutataja uongozi wa Mzee Mwinyi ndiyo ulioanzisha mfumo wa
Vyama vingi na kupanuka kwa haiba ya demokrasia, kuwepo kwa uhuru wa
vyombo vya habari lakini pia utawala wa Rais huyo ndiyo uliotanua wigo
kwa wananchi kujiajiri wenyewe katika sekta binafsi na kujitegemea.
Akizungumzungumzia
utawala katika awamu ya tatu alisema ndiyo awamu ilioendesha nchi kwa
msingi ya dhana ya uwazi na ukweli, kuwavutia wawekezaji, kupanuka kwa
sekta ya utalii, kuanzishwa kwa miradi ya elimu ya Mmem na Mmes,
kujengwa kwa daraja la mto Rufiji, miundombinu ya barabara na kubuliwa
kwa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambao uliinua sana maisha ya
wananchi masikini vijijini.
Shaka
akiizungunzia awamu ya nne chini ya Rais mstaafu Dk Jakaya Kikwete
alisema ndiyo iliboresha miundombinu ya barabara zinazoiunganisha mikoa
yote nchini huku takwimu zikionesha kipindi chake ndicho ambacho
barabara nyingi za lami zilijengwa
"Serikali
ya Dk Kikwete ilisimamia vyema ujenzi wa shule za kisasa za sekondari,
chuo kikuu kikubwa barani Afrika cha Udom, kuibuka vyuo vikuu vingi vya
serilaku na binafsi huku katika kila Kata kukiwa na sekondari,
hospitali, vituo vya afya na zahanati" Alieleza Shaka
Alieleza
utawala huo ndiyo ambao uliiweka katika chati nchi yetu kimataifa,
kulijenga madaraja makubwa ya Kigamboni, Simiyu na Malagarasi, viwanja
vya ndege vya Songwe na Mafia huku daraja la Kilombero likiwa limeachwa
kwenye hatua za mwisho katika ujenzi wake ikiwemo utoaji ajira nyingi
katika sekta za elimu na Afya.
Kaimu
Katibu Mkuu huyo alisema awamu ya tano ambayo inayoongozwa na Rais Dk
John Pombe Magufuli ikiwa na miaka miwili madarakani, ndiyo inayofanya
maajabu katika kupambana na vitendo vya ufisadi, kukomesha rushwa,
kusimamisha nidhamu ya kazi, uwajibikaji, kununua ndege , kujenga reli
kwa kiwango cha kimataifa na awamu hiyo ambayo haitasahauliwa na
watanzania kwa kupigania maslahi ya umma na kushamirisha uzalendo .
"Awamu
ya tano ndiyo mwisho wa reli, kama mtu alisafiri kwa treni toka Dar es
Salaam, hapa Kigoma ndiyo mwisho wake, Rais Dk Magufuli ni mwiaho,
amefanya ya kufanta na atazidi kufanya maajabu na kuiletea nchi mageuzi
hatimaye kuwa pepo mpya katika uso wa dunia na Afrika " Alisema Shaka
huku akishangiliwa.
Aliwataka
wananchi kuipa ushirikiano Serikali ya Rais wa awamu ya tano katika
dhamira ya kusimamia matumizi bora ya rasilimali, kukuza haiba ya
uzalendo lakini pia katika juhudi za kufanya nchi yetu kuwa ya viwanda
na yenye uchumi wa kati.
Jumla ya wanachama 24 toka vyama vya Chadema,
NCCR-Mageuzi, UDP na CUF kwa hiari na uamuzi wao walijiunga na CCM
katika mkutano huo wa ndani na kukabidhiwa kadi mpya za CCM na jumuiya
zake.
Kaimu
huyo katibu mkuu wa anaendelea na ziara yake ya kikazi katka wilaya za
Kigoma Mjini ,Buhingwe, Kigoma vivijini, kasulu na Kakonko kabla
hajahitimisha ziara hiyo Mkoani humu na kuelwkea mkoani mwanza