DK MAGUFULI APUNGUZA HEKA HEKA 2020

Image result for MAGUFULI


 Mwandishi Wetu,Kigoma


Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) umesema Rais John Magufuli kwa asilimia kubwa amekilpunguzia hekeheka na pirika za uchaguzi chama chake  na sasa njia ya ushindi ya chama hicho ni nyeupe na kinajiandaa kuongiza tena dola mwaka 2020.

Pia Umoja huo umewataka viongozi na wanachama wa CCM  kutobweteka na uhakika huo badala yake wajitume kwa bidii,kufanya kazi ya kisiasa  kisayansi, kizalendo kwa kuwatumikia wananchi mijini na vijijini.

Tamko hilo limetamkwa  jana na Kaimu, katibu mkuu wa uvccm shaka Hamdu Shaka alipozumgumza  na wanachama na viongozi wa matawi, kata na wiaya kwenye ukumbi wa CCM katika kata ya Kazuramimba wilaya ya Uvinza mkoani. hapa.

Shaka alisema utendaji wa serikali ya Rais huyo ndani miaka iliopita licha ya kukubalika kwa wananchi umeitikisa dunia huku wananchi wanyonge nao sasa wakijiona wakithaamianiwa, kuheshimiwa na kutetewa haki zao.

Alisema kazi kubwa inayofanywa na kiongozi huyo inastahili kuigwabkwa vitendo , kuungwa mkono,kupongezwa na kuthaminiwa kwasababu amedhairia kuwatumikia wananchi kwa nguvu. busara na maarifa yake.

"Dk Magufuli ametupunguzia hekaheka na kazi nzito  ya kusaka kura za ushindi wa mwaka 2020, hata hivyo nawahimiza viongozi na wanachama wa ccm tusibweteke na kujiamini,wajibu wetu kufanya kazi na kuwatumikia wananchi "Alisema Shaka .

Aidha aliwaeleza wananchi wa kata kuzuramimba kwamba chini ya serikali ya ccm hawataweza kujutia uamuzi wao kuchagua ccn wala kumuweka madarakani Rais Magufuli ambaye sasa ameamua kuwatumikia wananchi wote bila kuwabagua kwa itikadi za kisiasa. 

Kaimu huyo katibu mkuu alisema aliwataka vijana wa Mkoa wa Kigoma kuitumia vyema miundombinu ya barabara na reli katika kufanya biashara, shughuli za klimo na uvuvi ili kupambana na kadhia ya ukosefu wa vipato kiuchuni na umasikini .

Hata hivyo shaka aliitaka halmashauri za wilaya kufanya kila linalowezekana kupeleka asilimia 10 katika makundi ya Wanawake na vijana vijijini na kwanba halmashauri itakayozembea kutekeleza wajibu huo itajiekeza. 

"Halmshauri itakayishindwa kupeleka asilimia kumi kwa wananchi vijijini na mijini hatutaisamehe,watatubeba na kutuelekeza kwanini qashindwe kutimiza wajibu huo "Alieleza shaka huku akishangiliwa .

Katika mkutano huo jumla ya wanachama wapya 243 toka vyama vya upinzani vya  Chauuma,  Chadema, ACT Wazalendo ,CUF,NCCR -Mageuzi, DP na SAU waliorudisha kadi zao na kupewa mpya za ccm na katibu huyo wa uvccm. 

Katika msafara huo wa ziara ya siku tano Mkoani humu  Shaka anafuatana na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kigoma Peter Masanjira, Katibu  wa CCM Mkoa wa Kigoma Naomi kapambala na  Mbunge wa vijana Mkoa wa Kigoma Zainab Katimba .

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post