Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Umoja
wa Vijana wa CCM umesema siku za uwakilishi za Mbunge wa Kigoma Mjini
Zitto Kabwe zinahesabika kwani wananchi watampata somo maalum ifikapo
mwaka 2020 kwasababu ameshavunja mkataba kati yake na wananchi
waliompatia dhamana ya kuwatumikia hivyo toka sasa atazamwena tu
kupuuzwa.
Aidha Umoja huo
umesisitiza kwasababu mbunge huyo ana historia na kujifanya kujua
kwingi, kutoshaurika na kutopenda ushirkiano na wenzake kuna kila ishara
zinazoonyeaha atasombwa na mvua ya kisiasa na kutupwa kwenye maporomoko
ya Ziwa Tanganyika.
Matamshi
hayo yametamkwa jana na Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka alipokuwa
akizungumza na viongozi wa Matawi, Kata na wilaya na wanachama wa CCM
na jumuiya zake katika kata ya Gungu wilaya ya Kigoma Mjini .
Shaka
alisema mwanasiasa huyo ana historia ya hovyo ya kutofahamiana na
wanasiasa wenzake toka akiwa chuo kikuu Dar es salam , alipojiunga
Chadema akafukuzwa na sasa hawivi na wenzake huko ACT Wazakendo.
Alisema
kulikuwa hakuna sababu hata moja ACT Wazalendo chini ya uongozi wa
Zitto kupitisha maamuzi ya kumvua wadhifa aliyekuwa Mwenyekiti wake Anna
Mghwira kwasababu tu ya kuteuliwa na Rais Dk John Magufuli kuwa Mkuu wa
Mkoa Kilimanjaro .
"Siku
zake mtu huyu za kubaki katika uga wa siasa zimegota , hatabaki katika
uso wa siasa , naamini atasombwa na mawimbi ya Ziwa Tanganyika na
kufutika kurasa za siasa, haambiliki, mbabe na hapendi maelewano na
wenzake, mwaka 2020 atakiona cha mtema kuni "Alisema Shaka.
Alisema
kiongozi huyo Mkuu wa ACT Wazalendo ni mtu asiyefahamika kwakuwa leo
anaweza kusema jambo hili ukamuona kama mzalendo halisi laikini kesho
akageuka na kusema mambo yanayoonyesha ni mwanasiasa mtata na mtatanishi
.
"Nawaomba sana
wananchi wa kigoma endeleeni kuiunga mkono ccm na ssrikaki yake katika
kuendeleza amani, maendeleo, umoja na mshikamano, acheni kughiibiwa na
kughilibika kwa mambo ya kupita , chama chenu ni ccm hivyo vingine ni
kampuni binafsi za vigogo wa vyama hivyo 'Alisema
Shaka
aliwataja wanasiasa wakongwe akiwemo aliyekuwa Waziri katika Serikali
ya kwanza ya Tanganyika huru Marehemu Sheikh Amri Abeid Karuta na mmoja
kati ya waasisi 17 wa chama cha TANU hayati Mzee Saadan Abdul Kandoro na
wanasiasa wengine walisaidia sana katika kupigania Uhuru pia wapo
walioshiriki na kufanikisha Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
Vike
vike shaka aliwataka wanachama wa CCM kujichuja, kuwabaini na kisha
kuwatimua wanachama wasaliti wenye ndimi mbili ambao mchana huvaa sare
za ccm na kuiba mikakati na siri za chama lakini usiku watu hao
hubadilika na kujivika magwanda .
"Mwanachama
atakayebainika kwa ushahidi kamili ameshiriki kutenda usaliti atimuliwe
, Chama Cha Mapinduzi hakina tena njaa ya wanachama hivyo mtu
atakayeyumba au kuonyesha unafiki lazima aondoke kama wengine
walivyofukuzwa "Alisisitiza Shaka
Kaimu
huyo Katibu Mkuu alisema usaliti ni jambo baya na ovu lisilovumilika
kwani kama watu wa aina hiyo wangekuwepo nyakati za kupigania uhuru na
kupanga mbinu za kufanikisha mapinduzi, mambo yangekwama hatimaye
usultan na ukoloni ungelibaki hadi leo .
Hata
hivyo kaimu katibu mkuu huyo alifanya harambee ya papo kwa papo ya
kufanikisha ujenzi wa ofisi ya ccm kata ya Gungu ambapo wanachama na
viongozi walichangia jumla ya shilingi 355,000 huku mbunge wa vijana
Mkoa Kigoma Zainab Katimba akichangia bati mia moja.