MiSS Tanzania 2014 Lilian Kamazima akizungumza na waandishi wa habari kuelezea furaha yake baada ya kamati ya Miss Tanzania kumvisha taji hilo kutokana na kujiuzuru kwa Sitti Mtemvu aliyekuwa Miss Tanzania, Kulia ni Hashim Lundega Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania. |
Mkurugenzi
wa Kamati ya Miss Tanzania akizungumza na waandishi wa habari wakati
akitangaza kujiuzuru kwa Sitti Mtemvu aliyekua Miss Tanzania 2014 baada
ya kuzuka Sintofahamu kuhusu Umri wake, Lundenga amesema Sitti Mtemvu
aliandika barua ya kujivua taji na kuiwasilisha kwa kamati ya Miss
Tanzania Novemba 5 2014 ambapo kamati hiyo imeridhia kujiuzuru kwake na
kumvua taji , Hivyo taji hili na majukumu ya Miss Tanzania sasa
yatachukuliwa na mshindi wa pili Lilian Kamazima aliyekaa kushoto katika picha
ambaye taratibu za Miss Tanzania zinamruhusu kuchukua jukumu hilo,
Hashim Lundenga ametangaza uamuzi huo wakati akizungumza na waandishi wa
habari kwenye hoteli ya JB Belmonte jijini Dar es salaam