Ticker

6/recent/ticker-posts

WALIMU ARUSHA WALIPWA STAHIKI ZAO

 Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akiwa anaongea na waandishi wa habari ofisini kwake

waandishi wa habari wakifatilia mkutano wa mkuu wa wilaya

Na Woinde Shizza,Arusha
Jumla ya tsh.154 milion zimepatiwa  waalimu 701 wa shule za msingi na sekondari kutoka kwenye fedha ambazo zilitakiwa kulipa posho za nauli na simu za madiwani wa jiji la Arusha.

Akiongea na wanahabari ofisini kwake jijini hapa mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro alisema kuwa kutokana na malimbikizo ya fedha za likizo,kufiwa,nauli, uhamisho waliokuwa wanadai walimu  kwa kipindi cha mda mrefu ndio maana tumeamua kuwalipa ili waweze kufanyakazi ya kufundisha watoto wetu kwa moyo.

Daqqaro alisema kuwa baada ya kikao na mkuu wa mkoa Mrisho Gambo na waalimu wa shule 48 za jiji la Arusha, na kuagizwa kuhakikisha walimu wanalipwa stahiki zao ndani ya wiki mbili na  agizo hilo tumelitiza na walimu wamelipwa fedha zao zote walizokuwa wanadai.

Alisema kuwa fedha zilizolipwa waalimu hao tumezitoa kwenye fedha zilizokuwa wakijilipa madiwani posho za usafiri na posho za simu na kuzielekeza fedha hizo kutatua kero ya waalimu na mwisho wa siku vijana wetu wapate elimu stahiki bila manung'unuko kutoka kwa waalimu.

''Hapa napenda tusiingize ushabiki wa kisiasa katika hili na tuache kuzusha maneno maneno yanayaashiria uvunjifu wa amani maana teari nimeshaanza kusikia maneno maneno yanazuka kutoka kwa madiwani sasa nasema ivi sisi tumeamua kutekeleza agizo la mkuu wa mkoa ,na kunakili madiwani wanadai kuwa wao walikuta fedha hizi zikilipwa na ndio maana wakaendelea kupokea nachotaka kusama kama kweli walikuwa na nia njema na wananchi kwanini wasizikate mapema mpaka wasubiri mkuu wa mkoa aje aone mambo haya akate ndio waanze kuongea maneno maneno''alisema DC Daqqaro.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano ipo kuhakikisha wananchi walio wengi wanaondolewa kero zao kwa wakati na kuondosha kabisa kero mbali mbali ndani ya jamii ikiwemo waalimu kupewa stahiki zao kwa wakati.

Akawataka waalimu hao kuhakikisha malengo ya mkoa kuongeza ufaulu yamefikiwa kwa kufanyakazi kwa moyo huku serikali ikiendelea kumalizia malalamiko mbali mbali ya waalimu wa mkoa wetu.

Malipo hayo ya waalimu 701 yametokana na agizo la mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwataka dc na mkurugenzi wa jiji la Arusha Athman kihamia kuhakikisha malalamiko ya waalimu walioyatoa kwenye mkutano wao yanatekelezwa ndani ya wiki mbili .



Post a Comment

0 Comments