Nabii
mkuu mheshimiwa Dr Geordavie akiwa anahubiri katika
hema
la kukutania ngurumo ya upako kisongo jijini Arusha hii leo
Nabii mkuu akiwa anaendelea na huduma ya sikuu kuu ya kukusanya hii leo
Nabii akiwa anamwaga upako kwa waumi waliouthuria katika siku kuuu hii ya kukusanya hii leo (picha na Woinde Shizza,Arusha )
Nabii mkuu mheshimiwa Dr Geordavie akiombea bajeti mbalimbali za waumini walizoziletwa kwa ajili ya kutolewa neno la unabii hiii leo
Nabii mkuu mheshimiwa Dr Geordavie akiombea bajeti mbalimbali za waumini walizoziletwa kwa ajili ya kutolewa neno la unabii hiii leo
Habari picha na woinde shizza,Arusha
Watumishi wa madhehebu
mbalimbali hapa nchini wametakiwa kujijengea tabia ya kuwasaidia yatima ili nao
waweze kujisikia kama wao ni sehemu ya jamii
Hayo yamebainishwa leo na Nabii mkuu mheshimiwa Dr Geordavie
wakati akifanya dua maalumu ya kupitisha
bajeti ya watu walioshiriki katika sikukuu ya kukusanya iliyofanyika katika
hema la kukutania ngurumo ya upako kisongo jijini Arusha.
Alisema kuwa ni wajibu wa kila mtumishi kukusanya na kutoa kile alichonauwezo nacho ili kuweza kuwasaidia watoto yatima ,wananchi
wasiojiweza ili kuweza kuwafanya nao
wajisikie ni sehemu ya jamii
Alisema kuwa mbali na watoto yatima pia aliwasihi makanisa
ambayo yanajiweza kuweza kusaidia yale ambayo ni machanga ili kuweza kuwapa
nguvu ya kuweza kuendelea kueneza injili na kumtangaza mungu kupitia makanisa yao .
Nabii mkuu Dr Geordavie alisema kuwa kuwa lengo la sikukuu hii ya kukusanya
nikuwasaidia watoto yatima kwa kuwapa chakula kama mchele, sukari pamoja na
mafuta yakupikia ili nao wajisikie wanafuraha haswa katika kipindi hichi cha
sikukuu.
Alisema kuwa licha ya
misaada hiyo kwenda kwa watoto yatima, pia atatoa fedha kwa watumishi wa mungu
wenye makanisa madogo hapa nchini lengo likiwa ni kuinua huduma zao na
kuwasaidia katika kuendeleza huduma zao ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kanisa,
ununuzi wa vyombo vya muziki na shughuli nyingine za kanisa.
Sikukuu hii ya kukusanya huadhimishwa na huduma ya Ngurumo ya Upako
Duniani tarehe 26 ya kila mwaka, watu hutoa sadaka ya vitu mbalimbali ikiwemo
fedha kwa mujibu wa maelekezo ya Nabii Mkuu na kisha hugawanywa kwa vituo vya
watoto yatima huku fedha zikigawanywa kwa watumishi waliotuma
maombi ya kupata msaada wa kuendeleza
huduma zao.
Mwaka jana msaada wa zaidi ya shilingi milioni 15 ulitolewa
na waumini wa kanisa la Ngurumo ya upako na kugawanywa katika vituo mbalimbali
vya watoto yatima huku fedha zikigawiwa kwa baadhi ya makanisa madogo kwa ajili ya kuwasaidia mambo mbalimbali .
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia