Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI KUANZISHA TUZO ZA BLOGGER


Na Woinde Shizza,Dar es salaam


Waandishi wa habari za mitandao ya kijamii pamoja na wamiliki (Blogger) wametakiwa kutumia taaluma kukosoa ,kushauri mapungufu yaliyopo katika serikali ,kufichua maovu yanayofanywa na watumishi wa serikali ili kuweza kutengeneza Tanzania inayotakiwa.


Hayo yamebainishwa leo na waziri wa habari utamaduni na michezo Nape Nnauye wakati akifunga mkutano mkuu wa mwaka wa umoja wa wamiliki na waendesha mitandao ya kijamii (Tanzania Blogger Network ) na mafunzo ya siku mbili kwa wanachama wa TBN yaliyokuwa yakifanyika katika ukumbi wa PSPF jijini Dar es salaam.


Alisema kuwa wamiliki wa mitandao ya kijamii wanatakiwa kutumia taaluma yao na mitandao hii ya kijamii vyema katika kusifia ,kukosoa na kufichua maovu yote yanayofanywa iwe na serikali au watumishi wa serikali .


Aliwasihi wamiliki hawa kufanya zaidi habari za uchunguzi zinazoegemea katika vitu muhimu kama kilimo ,viwanda na biashara. 


''unajua blogger zinasomwa sehemu mbalimbali na nchi mbalimbali iwapo waandishi hawa wataandaa habari kama za uchunguzi mfano kuwe na watuwanaoandika habari za uchunguzi na kubezi katika sehemu moja kama vile kuandika habari za afya ,elimu na ata kilimo''alisema Nnauye


Aidha alisema kuwa mbali a hivyo Serikali imejipanga kuanzisha tuzo za waandaaji wa habari wa mitandao ya kijamii (Blogger)ambapo mchakato umeshaanza na wanatarajia tuzo kuanza mwakani


Alisema kuwa pia katika mashindano haya wanatarajia kutoa zawadi nono ambazo zitawapa motisha wa kushiriki mashindano haya .

Post a Comment

0 Comments