TEMBO, simba, chui, fisi na nungunungu kutoka Hifadhi ya Taifa ya
Wanyama ya Serengeti wamesababisha hasara inayofikia Sh bilioni 1.3
kwa kuvamia makazi ya wananchi i na kuharibu ekari zipatazo 6,000 za
mashamba, kujeruhi na kuua mifugo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira wilayani
Serengeti, Michael Kunani, alisema hiyo ni kwa mujibu wa uchunguzi
wa matukio ya wanyama hao uliofanyika kipindi cha kuanzia mwaka 2009
hadi 2016.
Alisema uchunguizi huo umebaini kuwapo na uharibifu wa mazao,
mauaji ya mifugo ambako wastani wa watu watatu huuawa kila mwaka
katika vijiji vya Robanda, Singisi,Makundusi na Nyamatoke.
Matukio hayo i hutokea wanyama hao wanapofika katika makazi ya
wananchi na baadhi ya watu wanapokwenda kufanya ujangili katika maeneo
ya uhifadhi, alisema.
“Mwingiliano huo wa binadamu na wanyamapori umesababisha kubadilika
kwa tabia za wanyama hao kama tembo kwenda na kubomoa nyumba na
kuangusha vihenge vinavyohifadhi nafaka hivyo kuongeza hasira kwa
wananchi.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia