Mwandishi wa Habari wa ITV na Redio One Khalfan Liundi (Mwenye
shati jeupe) akitoka katika kituo cha Polisi cha Usariver Mara baada ya
kupata dhamana,alikamatwa kufuatia amri ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru
Alexender Mnyiti kwa kutuhumiwa kuandika habari za uchochezi
Mwandishi wa Habari wa ITV na Redio One Khalfan Liundi (Mwenye
shati jeupe) akitoka katika kituo cha Polisi cha Usariver Mara baada ya
kupata dhamana,alikamatwa kufuatia amri ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru
Alexender Mnyiti kwa kutuhumiwa kuandika habari za uchochezi
Mwandishi wa Habari wa ITV na Redio One aliyekua
ameshikiliwa na jeshi la polisi wilaya ya Arumeru na kuwekwa mahabusu kwa zaidi ya masaa 24 kwa kile
kinachodaiwa kuwa ni agizo la Mkuu wa
Wilaya ya Arumeru Alexender Mnyiti ameachiliwa kwa dhamana.
Liundi alikamatwa Disemba 21 majira ya saa 8 mchana ambapo
awali alifunguliwa shtaka la kuandika habari za uchochezi ,ambalo hata
hivyo katika hali ya sintofahamu leo
asubuhi polisi katika kituo cha Usariver walikanusha kwamba hakukuwa nan
shitaka lolote isipokua wanafuata agizo la mkuu wa Wilaya la kumuweka mahabusu.
Akizungumza mara baada ya kuachiwa kwa dhamana leo majira ya
saa 9:30 alasiri Liundi amesema katika mahojiano na Askari wa upelelezi
ametuhumiwa kuandika habari nyingi zinazohusu malalamiko ya wananchi bila kile
kinachoelezwa kusikiliza upande wa Uongozi wa Wilaya.
Mwanasheria wa Mwandishi huyo kutoka Tume ya Haki za
Binadamu Edwin Silayo amesema Liundiameachiwa kwa dhamana ya Shilingi milioni
10 na wadhamini wawili huku akitakiwa kuripoti katika kituo hicho cha polisi
Disemba 27.
Tukio la kukamatwa kwa Liundi limewagusa Waandishi wa habari vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa ambao wameonekana
kusimamisha shughuli zao na kupiga kambi
katika kituo hicho kwa siku zote mbili.