Mkuu wa Wilaya ya Babati Raymond Mushi. |
Nchi kama
Tanzania itaendelea kubaki nyuma katika uwekezaji kama haitowatumia wataalamu
wenye fani katika uzalishaji ,hivyo Vyuo vya ufundi nchini vimeshauriwa
kuboresha mitaala ya masomo yanayofundishwa ili kuzalisha wataalamu
watakaoweza kuzalisha bidhaa bora nchini
zitakazoingia katika Soko la ushindani na kuifanya Tanzania kujivunia.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Babati Bw. Raymond Mushi juzi alipokuwa akimwakilisha Mkuu wa mkoa huo Dokta Joel Bendera katika mahafali ya tatu ya chuo cha ufundi VETA yaliyofanyika wilayani humo ambapo alisema kuwa Mitaala hiyo ikilenga kutoa nafasi ya kujiajiri na kuajiri wengine maendeleo ya kweli yatafikiwa.
Alisema maendeleo ni mjumuisho wa vitu vingi mbalimbali wakiwemo watu na stadi zao ambapo unapompa mtu stadi za kazi kama vinavyofanya vyuo mbalimbali vya ufundi ambapo hutoa mafunzo kwa wanafunzi wao ambao tayari inakuwa wamepata maendeleo ya nchi yatakayosaidia kukuza uchumi wa viwanda katika nchi husika.
Mushi aliongeza kusema kuwa ili kufikia azma ya uchumi wa viwanda kwa mwaka 2015 watanzania wanatakiwa wawe na uchumi wenye ushindani na kuwa na watu wenye ujuzi wa kutosha kwani raslimali kubwa kuliko zote katika uzalishaji ni kuwa na watu wenye ujuzi.
“Lazima vijana wajitambue na kujitathimini lengo la wao kuwepo katika dunia hii, itawasaidia kujua kipi cha kufanya na kipi kisichofaa kufanywa na hatimaye kuwa na ndoto za maisha wayatakayo kuishi, kwakuwa elimu inasaidia kujenga misingi bora ya maisha.” alisema Mushi.
Mkuu wa Wilaya ya Babati Raymond Mushi akizungumza jambo katika Mahafali hayo. |
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Manyara Bw, Felix Ole Ndukai akizungumza katika Mahafali hayo. |
Mkuu wa chuo hicho Felix Ole Ndukai alisema kuwa chuo hicho kimekuwa kikiendesha mafunzo ya muda mfupi mafunzo ambayo yameisaidia jamii ya wana Manyara kupata elimu na stadi za kazi wengine wakiwa watumishi wa serikali na binafsi ambapo zaidi ya wanafunzi2,400 wamepata mafunzo mbalimbali kati ya hao 1,850 walipata mafunzo ya udereva pekee.
Mkuu huyo wa chuo aliyataja baadhi ya mafunzo ya muda mrefu kuwa ni Uhazili,uungaji vyuma, useremala,uashi, umeme, maabara, ufundi magari na mafunzo ya muda mfupi ni udereva wa magari na pikipiki, udereva wa gari za abiria,ushonaji,ufundi wa kitarakimishi(Computer maintenance).
Alisema chuo hicho pia kimeimarisha mahusiano mazuri na taasisi zilizoko mkoani humo na kuweza kutengeneza madawati 1,153 ya shule za msingi kwa ushirikiana na jeshi la Magereza mkoa, utengenezaji wa viti na meza jozi (seti)300 kwa shule za sekondari kwa kushirikiana na ofisi ya RAS mkoa wa Manyara jambo ambalo anajivunia.
Alifafanua kuwa katika mahafani hayo ya tatu jumla ya wanafunzi 80 wakiwemo wanawake 23 na wanaume 57 walihitimu mafunzo hayo kutoka katika fani za umeme(15),useremala(13),maabara(21) na ufundi magari (31).
Alitaja baadhi ya changamoto zinayokikabili chuo hicho kuwa ni upungufu wa mabweni,karakana na madarasa, uhaba wa nafasi ya mafunzo kwa vitendo viwandani,upungufu wa magari ya kufundishia udereva na upungufu wa walimu.
Wahitimu wakiimba Wimbo wa Pamoja wa kuaga.
Mkuu wa Wilaya Raymond Mushi akimkabidhi Cheti mmoja ya wahitimu
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia