Ticker

6/recent/ticker-posts

MASHINDANO YA SCOUT KANDA YA AFRIKA MASHARIKI YAFANYIKA ARUSHA







Skauti wa TZ na wengine wa nchi za Afrika Mashariki wakipita
mbele ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kambi ya mashindano ya
skauti nchi za afrika mashariki inayoendelea mkoani Arusha
Skauti Tz na wengine kutoka nchi za afrika mashariki
wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa ufunguzi rasmi wa kambi ya
mashindano inayoendelea mkoani Arusha
Skauti kutoka Kenya na wengine wa nchi za Afrika Mashariki
wakipita mbele ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kambi ya
mashindano ya skauti nchi za afrika mashariki inayoendelea mkoani
Arusha
.


Na Woinde Shizza,Arusha
Vyama vya scout kanda ya Afrika Mashariki vimekutana mjini hapa kuanza
mashindano ya  mascout  yenye lengo la kuwezesha vikosi vya scout
kushindana pamoja ili kujipima katika utekelezaji wa programu ya vijana ya
stadi za kiscout katika vikosi na jumuiya ya afrika mashariki ambazo
wamekuwa wakijifunza katika maeneo yao.

Akizungumza katika mashindano hayo yalioanza jana meneo ya kisongo jijini
hapa,kamishna mkuu wa chama cha skauti tanzania Rashidi Mchata alisema kuwa
mashindano hayo yameshirikisha  vijana wa kiscout kutoka nchi tano za
jumuiya ya afrika mashariki.

Mchata alisema kuwa mashindano hayo yatahusisha makundi ya mascout wadogo
,mascout wakubwa na masouti vijana  kutoka kila nchi yatashindana
kutengeneza stadi za kiskauti kwa kutumia mbinu zao ambazo wamekuwa
wakifundishwa katika vikosi vyao   kwa ajili ya kuwawezesha kuhudumia jamii
na kuwafanya wawe wazalendo.

"Vyama vya mascout kutoka jumuiya ya afrika tumekutana hapa arusha kwa
malengo matatu ikiwemo mashindano ,jukwaa la vijana mascout lakini pia
tumekuwa na mkutano mkuu wa makamishna wa skauti kutoka nchi za jumuiya na
hii inasaidia kwa pamoja kuhakikisha kuwa vijana wetu wanakuwa wazalendo na
kupitia haya mashindano tutaweza kuwapata washindi ambao wanawakilisha nchi
zao walizotokea"alisema Mchata.

Rehema Ramadhani mwanascout kutoka  dar es salaam ambae anawakilisha
tanzania katika mashindano hayo alisema kuwa mashindano hayo yanajumuisha
mambo yote waliokuwa wanafundishwa kuanzia ngazi ya wilaya na kwamba
yanawapa uzoefu wa stadi zao kutoka kwa mascout wa nchi nyingine za jumuiya
ya afrika mashariki.

Alisema kuwa katika vikosi vyao wamekuwa wakifundishwa mambo mbali mbali
ikiwemo utunzaji wa mazingira kama ilivyo kauli mbiu ya rais magufuli
lakini pia jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa mtu au jamii pale inapopata
janga na hivyo wanaamini kuwa wataiwakilisha tanzania kuwa mshindi katika
mashindano

Kwa upande wake mwenyekiti wa jukwaa la vijana wa  kiscout katika jumuiya
ya afrika mashariki Murtadhwa Abdallah alisema kuwa taasisi mbali mbali
zinatakiwa kujitokeza na kushirikiana katika kufadhili scout kwani vyama
hivyo vimekuwa vikikabikiwa na changamoto ya fedha hivyo kushindwa
kujiendesha vyenyewe.

Post a Comment

0 Comments