SERIKALI IMEPIGA MARUFUKU DILI ZOTE ZILIZOKUWA ZIKIFANYWA KATIKA MCHAKATO WA MANUNUZI


Image result for Dk. Ashatu Kijaji

SERIKALI imepiga marufuku dili zote zilizokuwa zikifanywa katika
mchakato wa manunuzi na kusema wahusika wa dili watambue serikali
haitamvumilia mpiga dili wala vishoka .

Ameyasema hayo katika kongamano la saba la Wataalam wa Bodi ya
Manunuzi na Ugavi linalofanyika Mkoani Arusha, Naibu Waziri wa Fedha na
Mipango, Dk. Ashatu Kijaji alisema ni vizuri kila muhusika wa manunuzi
asimame vizuri kuhakikisha kila fedha inayotoka ya serikali inakwenda
kufanya kazi iliyokusudiwa.

“Nataka nyie wataalamu muelewe wale wote waliozoea kupiga dili na
vishoka sasa basi hatutaki kuona hilo na tutafuatilia kweli kwa
kila fedha inayotoka ikafanye maendeleo kusudiwa,”alisema.

Dk. Kijaji alisema serikali imetenga 40%A ya bajeti inakwenda
katika miradi ya maendeleo na ndani ya  hizo asilimia 70 ya
fedha hizo zinakwenda kwenye manunuzi ya maendeleo, hivyo lazima
kusimamia vizuri eneo hili.

Alisema hawatamvumilia mtu yoyote atakayekwenda vibaya katika manunuzi
au mchakato mzima wa manunuzi na hata waliozoea 10% waache
mara moja.

“Hizo asilimia 10% hatutaki kusikia wala kuona na hili mmezoea muache
mara moja maana hamtabaki salama, tunataka kuona kama Shilingi mia
inakwenda barabarani inakwenda yote na ukaguzi utafanyika na kufanya
tathimini kuona kama fedha zote hazijaishia kwa vishoka na wapiga
dili,”alisema.

  Dkt.Kijaji alisisitiza wataalamu wafanye kazi kwa watanzania ili viwanda
vilivyokusudiwa vijengwe kweli, lakini kukiwa na watu wajanja wajanja
hakutakuwa na viwanda na hilo serikali haipo tayari kuona inaangushwa.

Kwa uande wake mwenyekiti wa Bodi ya Wataalamu wa Manunuzi na Ugavi (PSPTB), Dk.Hellen Bandiho, alisema vema wenye mazoea ya kupiga dili wakaacha mara moja maana wakiendelea nazo watakufa nazo.

“Tunataka kila mmoja lazima afanye kazi kwa kufuata maadili kama
umepewa tenda itumike ipasavyo na ukipatiwa fedha na serikali ifanye
kazi iliyokusudiwa.

“Bodi tutahakikisha wanaofanya manunuzi ya serikali wote wawe watu
wenye sifa na ikigundulikana mtu anakwenda kinyume na sheria ya
manunuzi na tunavyotaka sheria itachukua mkondo wake,”alisema.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Manunuzi na Ugavi,
Godfrey Mbanyi alisema katika kongamano hilo kauli mbiu yake ya mwaka
huu ni utawala bora katika mchakato mzima wa manunuzi.

Alisema kauli mbiu hiyo iende sambamba na kuangalia mchakato wote wa
manunuzi uwe wazi sio wa siri na uwe uwajibikaji na kusiwe na mambo ya
siri, lakini uwe shirikishi na wote wanaohusika kila kimoja ashirikishwe vema.

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.