Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya iringa Abeid Kiponza,mbunge wa viti maalumu mkoani iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wakiwa katika moja ya madarasa ya shule ya msingi Azimio wakati wa kujadili jinsi gani ya kutatua changamoto za shule hiyo
Mbunge wa viti maalumu mkoani iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akikagua miundombinu ya shule ya msingi Azimio sambamba na wananchi na viongozi wa shule hiyo.
Hili ni moja kati ya madarasa ya shule ya msingi Azimio ambalo lipo taabani kabisa na likiwa linakaribia kuanguka kutokana na kuwa na nyufa nyingi ambazo ni kubwa sana
Hili ni moja kati ya madarasa ya shule ya msingi Azimio ambao linaonekana afadhari kidogo na kuwashawishi viongozi mbalimbali kuketi na kujadili maswala ya kutatua changamoto za shule hiyo ambapo madarasa mengine yapo taabani kuliko hili.
Na fredy mgunda,Iringa
Mbunge wa viti maalum mkoani
Iringa Ritta Kabati anatarajia kukarabati shule ya msingi ya Azimio iliyopo
manispaa ya Iringa kutokana na uchakavu wa majengo hayo.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa
miundombinu ya shule hiyo mbunge Kabati alisema ni aibu kwa shule kongwe kama
hiyo kuwa miundombinu mibovu kama hiii.
Kabati aliongeza kuwa shule
hiyo imeharika hovyo na inahitaji msaada wa haraka kuikarabati kwa kuwa wananfunzi
wanasoma katika mazingira magumu na kudumisha elimu ya wanafunzi hao.
“Hii shule imeanza sawa na
siku niliyozaliwa mimi lakini ukiiangalia imechakaa na imechoka hivyo sina budi
kuanza kuikarabati shule hii kwa kuwa ni aibu kwangu haiwezakani shule ikawa
manispaa ya iringa halafu ikawa katika muundo huuu”alisema kabati
Aidha Kabati alisema kuwa
hadi kufikia siku ya ijumaa ya tarehe 23 mwezi wa kumi na mbili atahakikisha
anakarabati shule yote ili iwe katika
ubora unaotakiwa kama shule nyingine zilizopo manispaa ya iringa.
“Tunashule bora sana hapa
manispaa ya iringa lakini hii ya Azimio imekuwa katika hali mbaya sana ni
jukumu langu kama mbunge wa mkoa wa iringa kutatua changamoto mbalimbali
zinazoukabili mkoa wangu”alisema Kabati
Kwa upande wake mkuu wa
wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema haiwezekani shule ya azimio ikawa
katika mazingira mabovu ya miundombinu kama yale hiyo hadi kufikia siku ya
ijumaa atahakikisha anakarabati shule
hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Naye mkuu wa shule ya msingi
Willfrid Chotipembe alimshukuru mbunge wa viti maalum Ritta Kabati pamoja na
mkuu wa wilaya kwa kufika shuleni hapo na kuahidi kutatua changamoto
zinazoikabili shule hiyo.