BREAKING NEWS

Saturday, December 3, 2016

MAJALIWA :TUMIENI BIDHAA ZINAZOZALISHWA NA VIWANDA VYA NDANI

 Mwenyekiti wa Kampuni ya Lodhia Group  Bw. Arun Lodhia akimpokea Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ili kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa wakati alipofika kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
 Mwenyekiti wa Kampuni ya Lodhia Group  Bw. Arun Lodhia (wa kwanza kushoto waliokaa) akiteta jambo na Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo na Naibu waziri wa kilimo ,Mifugo na Uvuvi Mhe. William Ole Nasha wakati walipofika kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akikata utepe tayari kwa uzinduzi wa  kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
 Kutoka Kushoto (mwenye suti bluu) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lodhia Group  Bw. Sailesh Pandit,  Mwenyekiti wa kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia wakiongozana na  Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ndani ya kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
 Mwenyekiti wa Kampuni ya Lodhia Group  Bw. Arun Lodhia akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ili kuongea na hadhara iliyopo kwenye kiwanda hicho mara baada ya kuzindua kiwanda kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea machache mara baada ya kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akizindua jiwe la msingi katika kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lodhia Group  Bw. Sailesh Pandit akiagana na  Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa mara baada ya kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Mwenyekiti wa kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia akiagana na  Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa mara baada ya kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lodhia Group  Bw. Sailesh Pandit akisoma risala mbele ya Mgeni rasmi ambaye niWaziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ndani ya kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016. Picha zote Gadiola Emanuel

habari na  Woinde Shizza , Arusha.

 Halmashauri za majiji, manispaa na miji wametakiwa kutumia mabomba ya maji yanayozalishwa nchini badala ya kuagiza bidhaa hiyo toka nje ili kuweza kuvinufaisha  viwanda vya ndani.

               

Hayo yamebainishwa na waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa wakati akizindua kiwanda cha   kutengeneza mabomba ya Plastic ya maji yenye  ukubwa wa aina mbalimbali  (Lodhia Plastics ) kilichopo njiro jijini hapa.

Alisema kuwa haiana haja ya halmashauri  au majiji kuagiza bidhaa mbalimbali nje ya nchi  wakati  nchi yetu inaviwanda vya kutosha vya kutengeneza bidhaa hizo.



“Sioni sababu ya wahandisi wa Halmashauri na washauri elekezi halmashauri kushinikiza wakandarasi wa hapa Arusha kwenda kununua mabomba ya maji nje ya mkoa wakati hapa kuna kiwanda kama Lodhia ambacho kinatengeneza hizo bidhaa kwakweli hii labda iwe   ni chuki tu”alisema Majaliwa ambaye ameanza ziara ya siku nane mkoani Arusha.



Alisema ni muhimu kwa halmashauri kununua mabomba hayo kwa matumizi ya miradi ya maji na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wawekezaji wa ndani.



“Washauri wa miradi mbalimbali acheni chuki …waache wakandarasi wanunue bidhaa bora zilizothibitishwa na Shirika la Viwango la Taifa (TBS) na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO),” alisema.

Aidha alitoa mfano, kwa upande wa Mkoa wa Arusha kuna mpango wa kujenga mradi mkubwa wa maji utakaogharimu dola za Marekani milioni 200, na katika utekelezaji wake ni lazima watoe kipaumbele cha kutumia mabomba yanayozalishwa na kiwanda hicho.

Mradi huo ukikamilika unatarajiwa kumaliza kero ya maji kwa wakazi wa jijini hapa.

Alisisiza haoni umuhimu wa halmashauri na wakandarasi kununua mabomba kutoka nje ya Arusha au nje ya nchi wakati kuna mabomba yanayozalishwa na wawekezaji wazawa na yanakidhi viwango.

“Serikali  yetu itaendelea kuwaenzi na kuwalinda wawekezaji wote wa ndani ambao wamekuwa msaada mkubwa wa kutoa ajira ambayo ni janga kwa taifa na dunia kwa ujumla”alisema Majaliwa.

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Lodhia Group, Arun Lodhia, alisema serikali ichukue nafasi ya kuzungumza na wenye viwanda mara kwa mara ili kujua matatizo yao na kuyatafutia ufumbuzi.

Alisema viwanda chini ya kampuni hiyo, vinazalisha bidhaa nyingi zenye ubora lakini makampuni yanashindwa kununua na kupenda zaidi kununua bidhaa za nje.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Sailesh Pandit, alisema  kwamba wanashindwa kuuza mabomba ya maji na malighafi nyingine katika miradi mikubwa ya maji iliyopo mkoani Arusha.

Alisema wanashindwa kufanya hivyo licha ya bidhaa zao kuwa na TBS na ISO kutokana na hujuma wanazofanyiwa na baadhi ya wahandisi na washauri elekezi wa miradi.

“Imeshatokea mara kadhaa kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi kuzuiwa kununua mabomba ya maji kutoka Lodhia Plastics na badala yake hulazimishwa kununua mabomba kutoka nje ya mkoa hivyo kuwasababishia gharama za ziada,” alisema.

Kuhusu ajira, alisema kiwanda hicho kimetoajiri  Watanzania kati ya 1, 200 hadi 1, 300 lakini pia Watanzania zaidi ya 500 wananufaika kutokana na kushiriki katika utoaji wa huduma mbalimbali kiwandani hapo.

Alisema mtandao wa viwanda vinne vinavyomilikiwa na kampuni ya Lodhia Group wanalipa kodi wastani wa Sh. bilioni 20 kwa mwaka.

Kwa upande wao, baadhi ya makandarasi, Samuel Lugemalila wa Kampuni ya Vest Tanzania Ltd na Kastuli Mandange kutoka Fraju Group Ltd  na Maxmilian Iranghay  wa kampuni Wining Spirit Construction Ltd, walitoa ushuhuda kuhusu namna washauri waelekezi na watumishi wengine wanavyowakataza kununua bidhaa za Lodhia Plastics na kuwataka wanunue zinazotengenezwa nje ya mkoa.

Walisema kitendo hicho kinawashababisha kushindwa  kukamilisha miradi yao kwa wakati na kuwaongezea gharama kubwa.
Aidha waliiomba serikali kuondoa urasimu kwa wahasibu kulipa malipo kwa wakati licha ya miradi kukaguliwa na kupata cheti cha uhakiki wa kazi.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates