Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitembelea Mradi wa umwagiliaji katika kijiji cha Jobag wilaya ya Karau ,mradi uliojengwa kwa ufadhili wa shirika la Worl Vision
Na Woinde Shizza,Arusha
Watumishi wote
wa Serikali wametakiwa kuzingatia
uwadilifu na uwajibikaji katika utendaji wao wa kazi.
Hayo yameelezwa na Waziri Mkuu wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa Jana alipokuwa akiongea na watumishi wa wilaya na
halmashauri ya Monduli Mara baada ya kuzindua wodi ya mama wajawazito ya hospital ya wilaya ya Monduli.
Aliwataka watumishi wote wa serikali kuzingatia
uwadilifu,uwaminifu na uwajibikaji katika utendaji wao wa kazi ili dhana ya
hapa kazi tu ichukue sehemu yake.
Majaliwa alisema Serikali ya awamu ya
tano niyawawajibikaji,waadilifu katika sekta za umma .
Amewataka watumishi
wawasikilize,wawahudumie na kuwatumikia wananchi bila yakuweka ubaguzi wa aina
yoyote ile.
Hii itasaidia kuonyesha matokea bora
ya kila mtumishi kulingana na taaluma aliyonayo nakupelekea kuongeza ufanisi
zaidi serikalini.
Aidha amewataka viongozi wa
halmashauri kusimamia fedha za miradi ya maendeleo zinazopelekwa na serikali na
zikafanye shughuli ambazo zilipangiwa.
"Kila sekta katika halmashauri
ihakikishe inapanga majukumu yake nakuyatekeleza kadri inavyopaswa"alisema
Majaliwa
Aidha aliwataka wananchi kote nchini
iwapo atataka Huduma n a kuhudumiwa vibaya asisite kutoa taarifa katika vyombo
husika.
"Mwananchi yeyote ambae atapewa
huduma vibaya na mtumishi wa serikali
asisite kutoa taarifa sehemu husika ili
mtumishi huyo aweze kuchukuliwa hatua Kali"alisema majaliwa.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia