BREAKING NEWS

Monday, December 26, 2016

SAFARI YA MWISHO YA WANAHABARI NA ASKARI WA JESHI LA ULINZI KATIKA KITUO CHA KIBO KABLA YA KUELEKEA KILELE CHA UHURU.

Baada ya kupuumzika kwa siku mbili katika kituo cha Horombo kwa ajili ya kuzoea hali ya hewa ,safari ya kuelekea kituo cha mwisho cha Kibo ikaanza .
Safari ilivyoendelea hali ya hewa ilibadirika arikadhalika uoto wa misitu mifupi ulianza kutoweka kadri safari ilivyoenedelea.
Safari iliendelea kwa motto wa "Mdogo Mdogo".
Wakati mwingine  kulihitajika maneno ya faraja ili kufanikisha safari hii.
Eneo hili ndilo la mwisho katika Mlima Kilimanjaro kuona maji yakitiririka wakati wa safafri ya kupanda Mlima Kilimnjaro.
Kutokana na kubadirika kwa hali ya hewa ,washiriki wengine walivalia vizuia upepo,wenyewe walivipa jina "Shilawadu".
Baadae uoto wa misitu ukatoweka kabisa ,safari ikawa ni ya kupita katika eneo la jangwa likijulikana kama Saddle.
Safari iliendelea ya kufika kituo cha mwisho cha Kibo Hut.
Wenye kuhitaji Msaada ,walipata msaada.
Mapumziko kwa ajili ya kupata Chakula yalifanyika katika eneo la Saddle.
Safari iliendelea ikiambatana na mvua katika eneo la Jiwe la Okoyo.
Hatimaye Safari ya kutoka kituo cha Horombo ikafikia tamati katika kituo cha Kibo Huts.
Washiriki wakapata picha ya pamoja  kabla ya kupata mapumziko kujiandaa na sfari ya kuelekea Kileleni itakayofanyika majira ya saa 5 usiku.


Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates