Mbwa ni mnyama kama wanyama wengine ambao huweza
kupata magonjwa mbalimbali ambayo hupelekea kufa au kuwapa vilema vya
maisha. Mbwa ni kama binadamu yoyote tu ambaye akishambuliwa na magonjwa
basi anaweza kuwa dhaifu na kupelekea kupoteza maisha au kupona lakini pia
ni wanyama kama binadamu tu wengine ambao hata wakipatwa na baadhi ya
magonjwa basi wanaweza kustahimili na kupona kabisa.
Basi leo tutaangalia baadhi ya magonjwa yanayowapata
viumbe hivi vinavyopendwa sana na rafiki mkubwa wa binadamu. Kama ilivyo
kwa wanyama wengine na binadamu ugonjwa uanza kuonekana kutokana na dalili
flani ambapo ndio zinakupa taarifa za kuhisi kuwa mnyama huyu ni mgonjwa.
Lakini kuna baadhi ya magonjwa ukiona dalili zake basi unajua kabisa kuwa
ishatafuna sehemu kubwa na kupona ni majaaliwa na hali ipo hivyo hivyo kwa
wanyama kama Mbwa.
Tuanze na Huu leo
1:Parvovirus
Infection (Kwa kifupi uitwa Parvo)
Ugonjwa huu ni ugonjwa unaosababishwa na Virusi
ambapo mara nyingi hushambulia mbwa wadogo wenye umri wa kuanzia wiki sita
mpaka miezi sita. Ugonjwa huu ni moja ya ugonjwa mbaya sana kwa mbwa
kwasababu unapomuingia tu basi matumaini ya kupona kwa mbwa huyo ni madogo
sana kwasababu ni ugonjwa ambao ukimpata mbwa ndani ya masaa 24 unaweza
kupelekea kifo kwa mbwa huyo.
Ugonjwa huu husambulia sana mapigo ya moyo na kupelekea
mapigo ya moyo ya mbwa huyo kwenda mbio sana, na kumfanya hapoteze hamu ya
kula, joto kushuka sana.
Hizi ndio dalili kubwa sana za ugonjwa huu wa Parvo
ni Kuharisha damu, Kutapika, kukosa hamu ya kula, kupungua uzito ghafla.
Mara umuonapo mbwa wako ana dalili hizi basi unashauriwa kuwasiliana na
mtaalamu wako wa wanyama kwaajili ya ushauri na matibabu zaidi ijapokuwa
kama mbwa huyo hakuwahi kupatiwa chanjo ya Ugonjwa huo tokea utotoni basi
asilimia ya kupona ni ndogo sana kwa maana unapoona dalili za ugonjwa huu
basi ni dhahiri unakuwa ushamshambulia sana mbwa huyo.
Nini husababisha ugonjwa huu wa
Parvo?
Mara nyingi ugonjwa huu usababishwa na mbwa
aliyehathirika moja kwa moja na ugonjwa huu japokuwa kuna sababu nyingine
kama endapo mbwa aliyeathirika na ugonjwa huu anapojisaidia haja kubwa na
mbwa mwingine akapita kunusa basi mbwa huyo anakuwa anaambukizwa moja kwa
moja. Inasemekana virus vya ugonjwa huu vinauwezo wa kuishi kwenye udongo
kwa takribani mwaka mmoja na ugonjwa huu unaweza kuambukizwa moja kwa moja
kutoka kwa mbwa mmoja kwenda kwa mbwa mwingine.
Vilevile Ugonjwa huu unaweza kuletwa na viatu endapo
mtu amekanyanga kinyesi cha mbwa aliyeathirika na ugonjwa huu basi
anapoingia nyumbani au kwenye mazingira ya mbwa ni rahisi sana kuacha
virusi hivyo na ikumbukwe kuwa virusi hivi huishi kwa takribani mwaka mzima
kwenye udongo.
Unapohisi umekanyaga kinyesi au kitu chochote ambacho
kinaweza kuwa na virusi vya parvo basi unashauriwa kusafisha eneo hilo kwa
kutumia madawa ya kuua virusi kwaajili ya kujirinda na ugonjwa huo
hatari.
Vilevile Kutompa chanjo sahihi mbwa wako na kwa
wakati kunaweza kupelekea kusababisha mbwa wako kupata ugonjwa huo, Kama
unavyofahamu kuwa mbwa wanatabia ya kunusa kila sehemu endapo bahati mbaya
kanusa sehemu ambayo tayari kuna virusi vya ugonjwa huo na hana chanjo basi
ni rahisi kushambuliwa na virusi hivyo.
Tiba ni Ipi kwa Ugonjwa
Huu?
Inavyosemekana mpaka sasa hakuna tiba sahihi ya
ugonjwa huu lakini Mbwa anapozaliwa tu na kufikisha muda wa wiki moja hadi
mwezi unashauriwa kumpatia chanjo mbalimbali kwaajili ya kumkinga na
magonjwa kama haya na chanjo hio sio ya mara moja tu anapochomwa mwanzoni
basi unatakiwa kufata ushauri wa mtaalamu wa wanyama kwa ratiba tena ya
kurudia kumchoma chanjo katika kipindi kijacho.
Aina hizi za mbwa ndio aina rahisi sana kushambuliwa
sana na ugonjwa huu Rottweilers, Doberman Pinschers, Pit Bulls, Labrador
Retrievers, German
Shepherds.
Tukutane tena siku
ijayo.
Je umeipenda makala
hii?Basi unaweza kushare na Wenzako
Tu follow
instagram kwa jina la @lukazablog @lukazablog
@lukazablog
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia