MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya
Bandari Tanzania (TPA), Deudence Kakoko, amewataka wafanyakazi wa mamlaka hiyo
kufanya kazi kwa bidii ili kwenda kasi ya Serikali ya awamu ya Tano.
Akifungua
michezo ya Tano ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (INTERPORTS GAMES)
viwanja vya shule ya Sekondari ya Popatlal Tanga jana, Kakoko, alisema kila
mfanyakazi wa Mamlaka hiyo anapaswa kujua wajibu wake.
Alisema kasi
hiyo iende sambamba na uboreshaji wa utoaji huduma bandarini na kuwa kivutio
kwa wageni ili kuweza kuitumia kwa kushusha shehena zao bandari za Tanzania.
Michezo hiyo
inashirikisha wafanyakazi wachezaji kutoka Tanga ambao ni wenyeji, Dar es
Salaam,, Mtwara na Bandari za Ziwa.