Ticker

6/recent/ticker-posts

MAHAKAMA YAMFUTIA MASHTAKA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA UVCCM ARUSHA ,WAKATI HUO HUO JESHI LA POLISI LAMSHIKILIA


Image result for SABAYA OLE  LENGAI
katikati ni aliyewai kuwa  mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya akiwa anatoka mahakamani (picha na maktaba)
Na Woinde Shizza,Arusha
Mahakama ya hakimu mkazi mkoani Arusha imefuta kesi iliyokuwa inamkabili aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Uvccm mkoani hapa Lengai Ole Sabaya baada ya upande wa Jamhuri kusema kuwa haitaki kuendelea na kesi hiyo

Hakimu aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo Gwan'twa Mwangoka amesema kuwa shauri hilo lililetwa na serikali mahakamani hapo,hivyo mahakama imeona haja ya kuendelea na shauri hilo

Awali wakili upande wa Jamhuri Grace Makidenya aliwasilisha ombi mahakamani hapo la kuiomba mahakama kuiondoa kesi hiyo

Kwa upande wake wakili anayemtetea Sabaya amesema kuwa ipo mamlaka anayokuwa nayo DPP kuondoa shauri mahakamani hivyo kesi iliyokuwa inamkabili imefutwa hivyo hakuna kesi inayomkabili tena.

Wakati huohuo

Baada ya kufutiwa kesi na mahakama Lengai Ole Sabaya alikamatwa tena na polisi ,mwandishi wa habari hizi  alifanya  jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi mkoani hapa Charles Mkumbo na iliaweze kuzungumzia sakata la kukamtwa kwa Sabaya,Kamanda alisema kuwa hiyo ni teknikali za kisheria bali kesi ni hiyohiyo na jeshi la polisi linafanya taratibu zao na zikikamilika watamrudisha tena mahakamani

Miezi kadhaa iliyopita aliyekuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi ‘UVCCM’ Arusha, Lengai Ole Sabaya alishtakiwa kwa kosa la kujifanya ofisa usalama wa Taifa na kughushi kitambulisho cha usalama wa taifa.

Kesi hiyo imetolewa maaamuzi na mahakama ya hakimu mkazi Arusha leo December 14 2016 ambapo imemuachia huru Lengai Ole Sabaya baada ya upande wa Jamhuri kusema hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo

Post a Comment

0 Comments