WANAFUNZI wa Vilabu vya Umoja wa
Mataifa kutoka vyuo Vikuu na Shule za
Sekondari na Msingi kutoka Mikoa mbalimbali nchini wamekutana Tanga kujadili
mambo mbali mbali yahusuyo shughuli za Umoja wa Mataifa.
Wanafunzi
hao walijadili mambo hayo yakiwemo Demokrasia na Utawala bora Barani Afrika
pamoja na changamoto za Raia katika nchi zenye machafuko.
Pia
walijadili uchafuzi wa mazingira kwa nchi zenye viwanda na uharibifu wa
mazingira ya bahari kwa baadhi ya viwanda kumwaga sumu baharini.
Akizungumza
katika kongamano hilo, Mlezi wa (YUNA) Mkoa wa Kilimanjaro, Fransiss Shelutete,
amezitaka Serikali nchi za Afrika kuwachukulia hatua kali uchafuzi wa mazingira .
Mwenyekiti wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa (YUNA) nchini Rahim Nassir, akizungumza kwenye kongamano la vilabu vya umoja wa Mataifa lililowashirikisha wanafunzi vyuo vikuu na kufanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Wanachama wa vilabu vya Umoja wa Mataifa (YUNA) kutoka Mikoa mbalimbali nchini wakifuatilia kongamano lililohusisha wanafunzi wa vyuoni na Shule za Sekondari na Msingi na kufanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Tanga
Viongozi wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa UN kutoka Mikoa mbalimbali
nchini wakiwa katika picha ya pamoja na wanachama kutoka maeneo
mbalimbali nchini.