picha ikionyesha mbunge wa bunge la jumuiyaya Afrika Mashariki Benard Murunya akiapa bungeni (picha na Maktaba) |
MAHAKAMA ya Wilaya ya Arusha, imemtia hatiani Mbunge wa Bunge la
Afrika Mashariki (EALA), Benard Murunya, kwa kupatikana na hatia ya
matumizi mabaya ya madaraka alipokuwa Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya
Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).
Kwa sababu hiyo, mahakama hiyo imemhukumu kulipa faini ya Sh 700,000 au kwenda gerezani miaka mitatu.
Murunya aliyekuwa Mhifadhi Mkuu wa NCAA na wenzake watatu, walikuwa
wakishitakiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia
Serikali hasara ya Dola za Marekani 66,890 (Sh milioni 133.7).
Katika kesi hiyo namba 71 ya mwaka 2015, washtakiwa wengine ni
aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa NCAA, Shad Kiambile,
aliyekuwa Meneja wa Huduma za Utalii katika mamlaka hiyo.
Wengine ni Veronica Ufunguo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Usafirishaji
wa Anga ya Cosmos Salha Issa, ambao waliachiwa huru na mahakama hiyo
baada ya kupatikana hawana hatia.
Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Patricia Kisinda, alisema katika
kosa la kwanza ilimtia hatiani Murunya kwa matumizi mabaya ya
madaraka.
Hakimu alisema Murunya alishindwa kuithibitishia mahakama kuwa
aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, alimwagiza
kubadilisha usafiri badala ya kupitia Kampuni ya Cosmos, wasafiri kwa
Kampuni ya Antelop Tours.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia