Na Mwaandishi Wetu,
Jalada la lalamiko katika kesi inayomkabili mtumiwa ambaye ni
mfanyabiashara mwenye asili ya kiasia Abdulrazak Othman Mohamed (43)
kumshambulia na kumjeruhi kwa panga Katibu wa Msikiti wa Jumuiya ya
Wamakonde uliopo Mtaa wa Nyamwezi na Amani jijiji Dar es Salaam imekwama
kwa Wakili wa Serikali na haijafkishwa Mahakamani.
Abdulrazak alimshambulia na kumjeruhi Katibu wa Msikiti wa Wamakonde
Abdallah Saiwaad kwa kumpiga mapanga matatu kichwani, begani na mkononi na
kumjeruhi mwilini hadi kulazwa katika hospital ya Taifa ya Muhimbili jijini
Dar es Salaam.
Saiwaad akiwa na wajumbe watano wa kamati ya Msikiti Wamakonde (wiki tatu
nyuma )walifila dukani kwa mpangaji wa dula la Msikiti Abdulrazak kwa
ajili ya kufuatilia deni la kodi ya pango ambapo mtuhumiwa alidaiwa
kumshambulia na kumjeruhi Katibu huyo.
Baada ya kumjeruhi kwa panga, alitoweka hadi alipotiwa nguvuni na polisi,
kuchukukiwa maelezo katika kituo cha polisi Msimbazi baadae akapata dhamana
na sasa anaendelea na kazi yake ya kuuza duka katika Mtaa wa Amani na
Nyamwezi maeneo ya jangwani .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala RPC Salim Rashid ameiambia uhuru kuwa
shitaka hilo limeondoka mikononi mwa polisi na kwamba liko chini ya
dhamana ya Ofisi ya Wakili wa Serikali kanda ya Dar es salaam hivyo hajui
kinachoendelea.
"Tumekamilisha jukumu letu kama polisi, jalada la kesi liko ofisini kwa
Wakili wa Serikali Kanda ya Dar es Salaam kwa hatua zaidi, sina uwezo wa
kulizungumzia jambo hilo kwani haliko tena katika dhamana ya polisi
"Alisema Kamanda Salim.
Juhudi za kumpata Wakili wa Serikali Kanda ya Dar es salaam zilishindikana
baada ya kutokea ishara za urasimu katika ofisi yake huku baadhi ya
wahudumu wakionekana kumkatisha tamaa mwandishi aliyefuatilia shauri hilo
ili kujua hatma ya kesi hiyo.
Baadhi ya waumini katika Msikiti wa wamakonde wameelezea kusikitishwa kwao
na maendeleo ya ukimya wa kesi hiyo huku aliyejeruhi akiendelea na shughuli
zake kama kawaida licha ya kukabiliwa na shitaka la kudhuru kwa kutumia
silaha.
Siraji Mfaume Idd (34)mkaazi wa Mtaa wa Muhoro alisema kinachoendelea ni
aibu kwa kwa waislam na vyombo vya sheria kuona mtu amepigwa, ameumizwa
kinyume na ubinadamu akikosa utetezi wa haki na aliyedhuru akidunda mitaani.
Alisema kitendi hicho kimewahuzunisha waumini wa Msikiti wa Wamakonde kwa
kushuhudia haki ikitaka kubakwa na kuwekwa mfukoni bila ya sababu za
msingi huku Baraza la Waislam Tanzania (BAKWATA )likiwa kimya bila
viongozi wake kupigania haki ya kiongozii wa Msikiti .
"Waislam hatuna mtetezi zaidi ya kumtegemea Allah, angepigwa muumini
mwingine aidha kanisani au kwenye hekalu, haki ingepatikana na hatma ya
uamuzi wake kwa mujibu wa sheria ungefahamika "alieleza Siraj.
Hemed Halfan "Killer" anayeishi Mtaa wa Ndovu alisema kuzorota kwa shauri
hilo na kutosikilizwa huku aliyejeruhi akifanya biashara kama vile
hakutenda kosa katika eneo ambalo ni miliki ya Msikiti kwa kudaiwa kodi
ni udhaifu wa kamati ya Msikiti na viongozi wa BAKWATA Mkoa wa Dar es
salaam .
Hemed alisema itakuwaje Katibu wa Msikiti apigwe , aumizwe na ajeruhiwe na
mpangaji halafu wajumbe wa kamati ya msikiti wakae kimya kama is uzandiki
na kukosa umoja.
"Wajumbe wa kamati nafikiri wanazunguukana nwenyewebkwa wenyewe ili
kumsaliti katibu wa msikitini, mungu hatakubali hata siku moja haki iwe
batili na batili isimame kama sheria na ishara ya haki "alieleza Hemed.
Sheikh wa BAKWATA Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Salum alipotafutwa
ili kuelelezea hatma ya shauri hilo ilielezwa yuko safarini mkoani singida
kuhudhuria maadhimisho ya sherehe za Maulid ya kuzaliwa kwa kiongozi wa
dini ya kiislam duniani Mtume M.uhammad ('S. A.W)
Alipotafutwa Mwenyekiti wa Kamati ya Msikiti wa Wamakonde Ustaadh Kitwana
Abdulrahman simu yake ya kiganjani muda wote iliita bila kupokewa kwa muda
mrefu.