WAZIRI
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Moses Nnauye,
amejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF na kuusifu kwa huduma zake za
haraka.
Waziri
Nape, amejiunga muda mfupi baada ya kufunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa
Mtandao wa Bloggers Tanzania, (TBN), kwenye jingo la kitega uchumi la
Jubilee Towers linalomilikiwa na Mfuko huo jana.
Aidha washiriki wa mkutano huo nao pia walijiunga na Mfuko huo kupitia uchangiaji wa Hiari yaani PSS.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhiwa kadi yake ya uanachama iliyotengenezwa chini
ya dakika 15, Waziri Nape alisema, “Aise, kitambulisho change tayari,
hongereni sana kwa huduma za haraka, mimi sikujua kama mnafanya kazi kwa
kasi yanamna hii,” alisema Mh. Nape wakati akikabidhiwa kadi hiyo na
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi ofisini kwake.
Tangu
kujaza fomu, kupiga picha na kukabidhiwa kitambulisho hicho, Waziri
alitumia kiasi cha dakika 25 tu, ikiwa ni muda mfupi baada ya kufunga
mkutano huo.Nao
wanachama wa Mtandao wa Bloggers Tanzania, (TBN), waliokuwa wakishiriki
mkutano huo, wamejiungana PSPF, baada ya kupatiwa maelezo ya kina
kuhusu umuhimu wa kujiunga na Mfuko, kutkana na manufaa mengi ukiachilia
mbali kujiwekea akiba.
“Ukiwa
Mwanachama wa Mfuko, moja ya faida kubwa ni kujipatia bima ya Afya,
itakayokusaidia wewe na familia yako, nikiwa na maana ya mke/mume na
watoto,” alisema Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdyul Njaidi
katika mada yake aliyoitoa kwa washiriki kuhusu kazi za Mfuko huo.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Moses Nnauye, (wapili
kushoto), akipokea fomu ya kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa
PSPF, kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bw. Adam Mayingu, wakati
wa Mkutano Mkuu wa Mtandao wa Bolggers Tanzania, (TBN), uliomalizika
jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa TBN, Bw. Joachim
Mushi.
Waziri Nape, akipokea kadi yake ya kujiunga na Mfuko huo kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi.
Waziri Nape, akijaza fomu hiyo, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Mayingu na kulia ni Bw. Njaidi
Bw. Njaidi akitoa mada kuhusu kazi za Mfuko huo kwa washiriki wa mkutano wa TBN
Bw. Njaidi akitoa mada kuhusu kazi za Mfuko huo kwa washiriki wa mkutano wa TBN
Washiriki wa Mkutano wa TBN, wakijaza fomu, huku Bw. Njaidi akitoa maelezo zaidi kwa baadhi yao
Bw. Mayingu akimkabidhi zawadi Waziri Nape
Waziri
Nape, baadhi ya wafadhili wa mkutano kutoka PSPF, na NMB, wakiwa aktika
picha ya pamoja na baadhiya washiriki wa mkutano huo wa TBN
Mmiliki wa Blogu ya Libeneke la Kaskazini kutoka Arusha Bi. Woinde Shizza akijaza fomu za kujiunga na PSPF
Baadhi ya washiriki wakijaza fomu za kujiunga na PSPF
Waziri Nape akimkabidhi Bw. Seria Tumainieli kadiya kujiungana PSPF
Waziri akimkabidhi Bi. Veronika kadi ya kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF
Waziri akimkabidhi Bw. Gadiola Emmanuel kadi ya kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia