Ticker

6/recent/ticker-posts

SHAKA HAMDU SHAKA AZINDUA RASMI KAMPENI YA JOGGING UVCCM MKOANI KAGERA

 Kaimu katibu mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka wa katikati akiendeleza
zoezi la jogging pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM  Wa Uvccm Mkoa wa Karagwe
Ndg Yahaya Kateme wa kwanza kushoto.
 Kaimu katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka wa pili kulia akiendelea
na Zoezi la Unyooshaji wa Viungo pamoja na Mkuu wa Mkuu wa Wilaya ya
Karagwe Mhe. Godfrey Ayub  Mheluka

 Kaimu katibu Mkuu Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi Taifa Shaka Hamdu
Shaka akiruka Mchaka mchaka katika viwanja vya CCM Wilaya ya karangwe leo.


Kaimu katibu Idara ya Hamasa,Sera,Utafiti na Mawasiliano Ndg Mtemi
Slyvester Yaredi akiendelea na zoezi la kunyoosha viungo


Kaimu katibu mkuu Uvccm Taifa ndg Shaka H.Shaka leo amezindua rasmi kampeni
ya Jogging UVCCM yenye kauli mbiu ya 'MAZOEZI KWA AFYA' iliyozinduliwa
Kitaifa Wilayani Karagwe.Katika Mazozi hayo Kaimu katibu mkuu ameshiriki
jogging na Mazoezi Viungo akiongozwa na Mwenyekiti  Uvccm mkoa wa Kagera
ndg YAHYA KATEME,Mkuu wa Wilaya Karagwe  Mhe. Godfrey Ayub  Mheluka pamoja
na vijana na viongozi mbalimbali  Wa Chama na Serikali Wilayani humo.
Akiongea
mara baada ya Mazoezi hayo Ndg: kaimu katibu mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu
Shaka amewataka Makatibu wa UVCCM Ngazi za Wilaya Nchini kote kuzingatia
maelekezo yaliyotolewa tangu Mnamo tarehe 24 Mwezi Oktoba 2016 la kuanzisha
jogging Club alisema "nitumie fursa hii kuwapongeza sana kwa kutambua
umuhimu wa mazoezi, sasa Vijana lazima wawe wakakamavu na tayari muda wote
hatuwezi kuwa na taifa la vijana goigoi wasio jiweza kama ambavyo  hata
makamu wa Rais alivyounga mkono katika swala hili la mazoezi " Pia
amewataka vijana wote kushiriki ipasavyo Zoezi hili amesema '' Jogging ni
swala muhimu sana kwa vijana kwani pamoja na kujenga miili yetu jogging
itatufanya tuwe wamoja t wenye ushirikiano wa kudumu haswa katika mambo
mbali mbali ya kijamii''. Kaimu katibu mkuu yupo katika ziara ya siku nane
mkoani Kagera ambapo atatembelea wilaya zote 8 za mkoa wa Kagera.

Post a Comment

0 Comments