Na Mahmoud Ahmad Arusha
Suala la kuachiana viti vya kugombea udiwani,ubunge kwa umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA)bado
kizungumkuti katika Kata ya Mateves wilayani Arumeru ambapo CUF na CHADEMA wasimamisha wagombea
hali inayopelekea kugawa kura za wagombea hao wa Ukawa.
Akizungumza na wanahabari Ofisini kwake Mkurugenzi wa
Uchaguzi mkoa wa CUF Arusha Zuberi Mwinyi alisema kuwa wao wamesimamisha
mgombea kwenye kata hiyo kutokana na mgombea wao kukubalika kwenye kata hiyo
hivyo kuwataka wenzao kuwaachia kata hiyo kwani wanazo kata nyingi kwenye
maeneo hayo.
Mwinyi alisema kuwa Tulikuwa na makubaliano ya kuachiana
kata na nafasi za Ubunge lakini wenzetu vyama wenza bado wamekuwa na Tamaa ya
kusimamisha wagombea kila inapotokea nafasi wemekuwa mbele kusimamisha wagombea
bila kujali makubaliano hali inayopelekea sisi kama chama kuamua kusimamisha
mgombea wetu eneo hilo.
Alisema kuwa sisi kama CUF tumewaachia wenzetu wa chadema
kata zote za jiji la Arusha ambapo walishinda kata 24 na moja kuangukia
mikononi mwa chama cha Mapinduzi (CCM), ili hali wao wameshindwa kutuachia kata
hiyo moja kama wenza na kutusaidia kuweza kuwa na mwakilishi kwenye vikao vya
kutnga sera je huku ni kujenga umoja au kubomoa.
“Tulikuwa na makubaliano ya kuachiana kata na nafasi za ubunge
jambo hili limeonekana kushindikana kwa wenzetu kuwa na tamaa huku
tukiwadanganya wananchi kwa wimbo wa ukawa ukawa kumbe si hivyo wenzetu wapo
kimaslahi zaidi na uroho wa madaraka”alisema Mwinyi.
Akatanabaisha kuwa CUF lazima itachukuwa kata hiyo na kazi
ndio imeanza ya kuhakikisha kata inaingia mikononi mwetu tukiwa na lengo la
kukijenga chama kuhakikisha mwaka 2020 tunakuwa na viti zaidi vya udiwani na
ubunge katika jiji la Arusha na mkoa kwa ujumla.
Suala la mgawanyo wa maeneo ya kugombea limekuwa
likivichanganya vyama hivi licha ya kuwepo makubaliano yaliofanywa na vingozi
wa vyama vine hali inayoonekana kutokuwa na muafaka katika jambo hili, mfano
majimbo ya segerea chadema na cuf walisimamisha wagombea na kujikuta
wakiangukia pua katika jimbo hilo,hali inayoonyesha hakuna makubaliano katika
hilo.
“tumekuwa tukiongea kweye vikao bila hatua kuchukuliwa na
wenzetu wamekuwa waongeaji wazuri kwenye vikao bila utekelezaji hali
inayotuwiwa vigumu kukijenga chama na kuwa na viti vya wabunge na madiwani katika
mkoa huu kutoka na hila za wenzetu”alisisitiza Mwinyi
Juhudi za wanahabari kuwatafuta viongozi wa CHADEMA mkoani
hapa akiwemo Mwenyekiti wa chama na Katibu wa Kanda ya kaskazini wa chama hicho
Amani Golugwa ziligonga mwamba baada ya simu zao kutokupokelewa kila
walipopigiwa bado juhudi zinaendelea kuwatafuta ili waweze kujibu madai hayo.