MKUU WALAYA YA HANANG AWATAKA VIONGOZI WAKIJIJI CHA GERTANUS KUITISHA MKUTANO WAWANANCHI HARAKA ILI KUTOA MAONI JUU YA VIONGOZ WANAOSABABISA MIGOGORO YA ARIDHI

 Image result for MKUU wa Wilaya ya Hanang, Sara Msafiri,
mkuu wa wilaya ya Hanang, Sara Msafiri akifafanua jambo
 
Na Woinde Shizza, Arusha

MKUU wa Wilaya ya Hanang, Sara Msafiri, ameutaka uongozi wa Kijiji cha
Gidika kilichopo Kata ya Getanus, kuitisha mkutano mkuu utakaowapa
wanakijiji fursa kutoa maoni juu ya viongozi wanaodaiwa kusababisha mgogoro
wa ardhi.

Aidha alitaka aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji hicho, Deo Luizer na viongozi
wenzake, kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa kukiuka maamuzi ya ugawaji
wa ardhi.

Mgogoro huo umedumu kwa miaka mitano sasa.

Alitoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji hicho mwishoni
mwa wiki.

Alisema viongozi hao waliendesha zoezi la ugawaji wa shamba la ekari 3365
ambalo serikali kuu ilirudisha kwa wananchi kutoka sehemu ya shamba
lililokuwa chini ya Nafco.

Aliwataka viongozi hao kumpa mrejesho juu ya maamuzi ya mkutano ambao
ameagiza uitishwe.

“Hatuwezi kuendelea na viongozi ambao wanashindwa kuwajibika, halafu
wanakiuka maamuzi ya wananchi, hawa tunawaita wezi hawawezi kwenda na kasi
ya mabadiliko ya serikali hii ya awamu ya tano lazima wafikishwe katika
vyombo vya sheri.

“Shamba hili lilirudishwa kwenu na serikali kuu ili nyie wananchi muweze
kunufaika nalo lakini hati bado ipo serikali kuu kwa hiyo mkiendelea kuleta
vurugu juu ya shamba hilo serikali ina uwezo wa kuzuia hati yake,” alisema.

Alisema kama wanakijiji waliamua kuweka shamba hilo katika mipango ya
matumizi bora ya ardhi lakini viongozi wao walishindwa.

“Viongozi hao ndiyo waliotufikisha huku leo. Nafahamu mlipopewa shamba hili
mliweka matumizi bora ya ardhi mlitenga eneo la mifugo, mlitenga eneo la
kilimo na mkatenga Land bank,” alisema.

Alisema kiini cha mgogoro huo wa ardhi kinatokana na viongozi wa serikali
ya kijiji akiwemo Afisa Mtendaji wa Kata ya Getanusi, kukiuka makubaliano
ya mkutano mkuu  wa kijiji ambao uliridhia shamba hilo lenye hekari 3,366
kugawiwa kwa wananchi wa kijiji hicho cha Gidika.

Alisema mkutano huo uliridhia kila kaya ipewe hekari tatu jambo ambalo
halikufanyika badala yake baadhi ya kaya zilipewa chini ya hekari hizo na
kaya nyingine kukosa kabisa.

Pia alisema viongozi hao walikiuika makubaliano ya kutenga eneo la malisho
la  hekari 612, baada ya kujigawia jumla ya hekari 48 na kuuza jumla ya
hekari 186 ikiwa ni sehemu ya eneo la malisho ambalo kijiji kiliazimia
litengwe ikiwa ni mpango wa matumizi bora ya ardhi.

Alifafanua kuwa licha ya viongozi hao kujigawia na kuuza maeneo hayo kwa
manufaa binafsi viongozi pia walishindwa kubainisha na kuwagawa jumla ya
hekari 469.

Alisema hekari hizo kwa mujibu wa uchunguzi na upimaji uliofanyika katika
eneo hilo badod wananchi hawajagawiwa wala kuwekwa katika mpango wowote wa
matumizi bora ya ardhi ya kijiji.

Hata hivyo, Sara alisema kuna baadhi ya watu wanalima hekari hizo 469
lakini hawajachukuliwa hatua kutokana na kukingiwa kifua  na baadhi ya
viongozi.

Alitoa agizo la kuchukuliwa hatua viongozi hao ambao wamejunufaisha na
ardhi ya kijiji kwa kujichukulia hekari 703 kati ya 3,366 hivyo kupelekea
mgogoro uliodumu kwa miaka miatano sasa ndani ya kijiji.

Kwa upande wake kaimu afisa kilimo wa wilaya hiyo, Daniel Lyimo,
akibainisha namna matumizi ya eneo hilo yanavyopaswa akisema serikali
ilitoa sehemu ya shamba hilo kwa ajili ya wananchi wa Gidika.

Alisema kwa mujibu wa mihutasari ambayo wamepewa na kijiji hicho inaonyesha
mkutano mkuu wa kijiji uliazimia itengwe eneo la malisho la ekari 612, na
kila kaya katika kijiji wagawiwe kwa kupewa ekari tatu tatu.

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.