Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na
watumishi wa serikali na halmashauri
kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC),
Baadhi ya wafanyabiashara wa Arusha wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye Ukumbi wa Simba katika Kituo
cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha
Na Woinde Shizza,Arusha
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imepiga marufuku uchapaji holela
wa vitabu vya kufundishia na kujifunzia kwa wachapaji binafsi na badala
yake uchapaji huo utasimamiwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA) ili
kuthibiti ubora.
Amesema
mbali na kudhibiti wa ubora pia uamuzi huo unalenga kuwa na kitabu
kimoja kwa kila somo kwa kila mwanzfunzi kwa nchi nzima ili kuweka
uwiano mzuri katika ufundishaji na upimaji wa wanafunzi .
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Desemba 2, 2016) wakati akizungumza
na walimu wa halmashauri ya Jiji la Arusha na wilaya ya Arusha kwenye
Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) akiwa katika siku ya
kwanza ya ziara ya kikazi mkoani Arusha.
Ziara
hiyo inalenga kukagua utelelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM,Utendaji
wa Serikali, kusikiliza na kujionea kero zinazowakabili wananchi wa
Mkoa huo kwa kushirikiana na viongozi wa Mkoa ili kuweza kuzitafutia
suluhisho.
Amesema
kipindi cha nyuma vitabu vilikuwa vinachapwa na watu mbalimbali hivyo
kusababisha malalamiko makubwa kutokana na vitabu hivyo kuwa na makosa
mengi. “Sasa vitabu vikibainika kuwa na makosa tutaibana Taasisi ya
Elimu Tanzania,”.
Aidha,
amesema Serkali itahakikisha kila mtoto anakuwa na kitabu chake ili
kuwawezesha kusoma vizuri na kuwa na uelewa wa kutosha ikiwa ni pamoja
na kuwarahisishia walimu katika ufundishaji.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amezungumzia kuhusu madeni ya walimu, ambapo
amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kutenga fedha katika
mapato yao kwa ajili ya kulipa madai ya watumishi mbalimbali katika
maeneo yao wakiwemo walimu.
Awali
Waziri Mkuu alizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Jiji na wilaya
ya Arusha na kumuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Arusha kumchunguza Ofisa Utumishi wa wilaya ya
Arusha, Bi. Imelda Isosi kufuatia tuhuma za rushwa, ufisadi,
unyanyasaji kwa watumishi zilizotolewa dhidi yake.
Waziri
Mkuu alitoa agizo hilo baada watumishi hao kupewa fursa ya kumuuliza
maswali ambapo mhudumu wa Chumba cha kuhifadhia maiti wa Hospitali ya
Ortumet Wilayani Arusha, Bw. Bernard Mtei kudai kwamba halmashauri ya
wilaya ya Arusha inanuka ufisadi na rushwa hususan katika sekta ya afya.
Baada
ya kutoa madai hayo Bw. Mtei alimkabidhi Waziri Mkuu nyaraka mbalimbali
zenye uthibitisho wa madai hayo, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw.
Mrisho Gambo amuhakikishia Waziri Mkuu kwamba watafanya uchunguzi wa
kina dhidi ya tuhuma hizo na zikithibitika wahusika watachukuliwa hatua
za kinidhamu na kisheria
Wakati
huo huo Waziri Mkuu ameitaka Idara ya Uhamiaji kudhibiti wahamiaji
haramu kwa kuanza kufanya misako katika nyumba za kulala wageni ili
kuwabaini wageni wanaoingia nchini bila ya kibali kwani ni chanzo cha
kuingiza silaha haramu nchini.
Amesema
inashangaza kuona silaha za aina nyingi katika maeneo mbalimbali ambazo
Tanzania hakuna ambazo zinadaiwa kuingia nchini kupitia maeneo ya
mpakani. “Hivyo ni lazima Idara ya Uhamiaji ihakikishe wanadhibiti
uingiaji wa wahamiaji kwenye mipaka mbalimbali nchini,”.
Waziri
Mkuu amesema Serikali haizuii wageni kutoka mataifa mengine kuingia
nchini ila ni lazima udhibiti wa wageni hao ufanyike ikiwa ni pamoja na
kujiridhisha sababu za kuja nchini na muda watakao kuwepo.
Hata
hivyo aliwasihi watumishi wa idara mbalimbali za Serikali kuhakikisha
wanafanya kazi kwa nidhamu, weledi, uadilifu na kuwatumikia wananchi
wanaohitaji huduma mbalimbali hata kama wamekosea kuuliza katika maeneo
yao.
Amesema
“baadhi ya wananchi hawana uelewa juu ya wapi wapeleke malalamiko yao
lakini kwa kuwa wewe ni mtumishi wa umma unapaswa kumsikiliza na
kumwelekeza aende wapi badala ya kumtolea maneno yasiyofaa,”.
Aidha alitoa ruhusa kwa wachimbaji wakubwa wote kuagiza baruti za kulipulia migodi wenyewe ili kuweza kupunguza tatizo ambalo linawakabili .
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia