Ticker

6/recent/ticker-posts

MSANII WA FILAMU KAJALA MASANJA AACHILIWA HURU LEO!


Leo ndio siku hukumu ya kesi iliyokuwa ikimkabili muigizaji Kajala iliposomwa.Katika kesi hiyo Kajala alihukumiwa miaka nane jela au kulipa faini ya milioni 13.Hivi ninavyoandika Kajala yupo nje baada ya pesa hizo kutolewa na muigizaji mwenzake Wema Sepetu.
Katika kesi hiyo ambayo Kajala hakuwahi kupata dhamana alikuwa ndani muda wote.Machi 15, mwaka jana Kajala na aliyekuwa mumewe walifikishwa mahakamani wakikabiliwa na kosa la utakatishaji fedha haramu ambapo kwa mujibu wa sheria kosa hilo halina dhamana.
Washtakiwa hao walikuwakabiliwa na makosa matatu, kosa la kwanza ni la kula njama ambapo washtakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa kwa kuhamisha umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi Salasala jijini Dar es Salaam.Shtaka la pili ni ni kwamba Aprili 14 mwaka 2010 waliamisha isivyo halali umiliki wa nyumba hiyo kinyume na kifungu cha 34(2)A(3) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007. Shitaka la tatu ni la kutakatisha fedha ambalo walilitenda Aprili 14 mwaka 2010 huku wakijua ni kinyume cha sheria.
Kajala pichani walipocheza filamu ya DEVEL KINGDOM ya Kanumba pamoja na Noah Ramsey wa Nigeria.

Habari zaidi kesho katika movie leo na Zamaradi Mketema aliyekuwepo mahakama ya kisutu wakati hukumu hiyo ikisomwa!
Pia hongera Wema Sepetu kwa kumshika mkono msichana mwenzako dada!

Post a Comment

1 Comments

  1. Sijaipenda hiyo kabisa kama wema anadiriki kutoa pesa kwa watu ambao walijua nini wanafanya ni kama amekufuru kwa Mungu.Namuomba abadirike kwani hizo pesa atakuja kuzijutia pindi atakapoishiwa.Namshauri atembelee hospitalini na ajionee jinsi wagonjwa wanavyotabika kwa kukosa madawa.Pia atembelee vituo vya kulelea watoto yatima na ajionee jinsi wanavyoishi katika mazingira magumu.Atembelee vijijini ajionee jinsi wanafunzi wanavyosoma katika mazingira magumu ikiwemo ukosefu wa madawati.Namshauri abadirike kuriko kuuza sura kwa kujitangaza kwenye vyombo vya Habari.

    ReplyDelete

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia