Promota
Jay Msangi (katikati) akiwa na Bondia Mmarekani (kushoto) aliyekuwa aje
kupigana na Bondia Mtanzania, Alphonce Mchumiatumbo katika pambano hilo
la juzi.
****************************************
Na Mwandishi Wetu
Promota
aliyeandaa pambano la Kimataifa la ubingwa wa dunia la uzito wa super
middle kati ya bondia Francis Cheka na bondia kutoka Marekani, Phill
Williams, Jay Msangi wa kampuni ya Hall of Fame Boxing and Promotion,
anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Kati kwa tuhuma za
kumdhulumu bondia kutoka Marekani.
Kamishna
Msaidizi wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Ahmed Msangi
alisema jana kuwa promota huyo alikamatwa jana Jumamosi Mchana maeneo ya
Oysterbay na kufikishwa kituoni hapo kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.
ACP
Msangi alisema kuwa promota huyo alihojiwa na Polisi kituoni hapo na
kuendelea kumshikilia promota huyo hadi hapo uchunguzu wa suala hilo
utakapokamilika.
Alisema
mbali ya kumhoji promota huyo, pia waliweza kuchukua maelezo ya bondia
Mmarekani Williams na meneja wake sambamba na Rais wa Organizesheni ya
Masumbi Tanzania (TPBO)- Limited, Yasin "Ustadh" Abdallah na wadau
wengine waliohusika katika pambano hilo.
Aidha
Msangi alifafanua kuwa bondia Williams anadai jumla ya Dola za
Kimarekani 8,200,000 (sawa na shs (Milioni 14) za Kitanzania kwa mujibu
wa mkataba uliosainiwa baina yao.
"Jambo
linalodaiwa kufanywa na promota huyo ni aibu kubwa kwa Taifa, sisi
tulikuwepo katika pambano hilo ambapo tulishuhudia baadhi ya mabondia wa
Tanzania nao wakimalamikia huku wengine wakigoma kupanda ulingoni, kwa
kutolipwa pesa zao, ni aibu kwa Taifa mbele ya wageni waliokuja
kufanikisha pambano hilo ambalo Cheka alishinda kwa pointi," alisema
Msangi.
Katika
pambano hilo mwandishi wa habari hizi wa mtandao huu, aliwashuhudia
baadhi ya mabondia kama Alphonce Mchumiatumbo, Thomas Mashali, Mada
Maugo na Francis Cheka, wakigoma kupanda ulingoni kabla ya kulipwa pesa
zao walizosainiana katika mkataba wao.
Hata
hivyo, mabondia hao walipanda ulingoni baada ya kikao kilichoitishwa na
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara
kilichofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee. Kikao hicho kiliamua
kuwa promota Msangi kuweka rehani gari lake ambapo tayari mdau mmoja wa
ngumi za kulipwa nchini alikuwa tayari kutoa Dola 12,000 za Kimarekani
ili walipwe mabondia hao na wengine.
Promota
Msangi alifanya ujanja na kutotoa gari lake, hali iliyopelekea kutokea
matatizo makubwa ambayo yameiweka nchi katika aibu kubwa hasa katika
mchezo wa ngumi. CREDIT:SUFIANI MAFOTO BLOG
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia