MSANII WA KIKE WA FILAMU AJIVUNIA KUPIMA UKIMWI NA KUKUTA HANA MAAMBUKIZI

Msanii  wa  Bongo Movie, Rachel Haule ‘Recho’ amejikuta akivuja  jasho  la  furaha baada ya kupima Ukimwi na kujikuta yupo salama.
 
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni maeneo ya Sinza Palestina ambapo Recho alienda kupima katika Hospitali ya Amen iliyopo Sinza ambapo kabla hajapata majibu hayo alikuwa akihaha huku na kule kutokana na wasiwasi.
 
Baada ya vipimo hivyo, Recho alipewa majibu yaliyoonesha kuwa yupo salama kitu ambacho kilimsababisha acheke na kuwataka  wenye  wivu  wajinyonge.
 
“Namshukuru Mungu  kwa sababu nimejikuta mzima baada  ya  kupima  UKIMWI, Mwenye wivu  na  maisha  yangu  ajinyonge  tu,” alisema Recho.


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post