Halmashauri ya jiji
la Arusha imeingia matatani mara baada ya kudaiwa kuipatia mkataba kampuni
ya kuwasha taa za barabarani jijini hapa ya Skytell Ltd ihali kampuni hiyo ilimaliza mkataba wake
mwaka jana mwezi julai.
Mbali na kuipatia mkataba
huo wa mwaka mmoja pia uongozi wa jiji hilo umedaiwa kuchukua fedha kiasi cha
sh,5 milioni kama ada ya ushuru wa mabango kwa mwezi Agosti mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa
zilizolifikia gazeti hili zimedai kuwa uongozi wa jiji hilo uliipatia mkataba wa
mwaka mmoja kampuni hiyo mnamo Agosti 8 mwaka huu.
Taarifa hizo
zimeeleza kwamba katika mkataba huo nambari 0251
uliosainimwa na mhandisi mkuu wa jiji hilo,Afwilile Lamsy uliitaka kampuni hiyo kulipa kiasi cha
sh,70,444,800 milioni kuanzia mwezi julai 2013 hadi June 2014 kama ada ya mwaka
mzima.
Hatahivyo,taarifa za
uhakika zimedai kuwa kampuni ya Skytel
ilimaliza muda wake mnamo mwaka jana mwezi julai na hadi sasa hakuna zabuni yoyote
iliyofunguliwa ya kuwasha taa za barabarani jijini Arusha.
Vyanzo vya habari
vimedai kwamba uongozi wa jiji la Arusha kwa sasa ndiyo unausimamia mradi wa
taa za barabarani jijini hapa hadi pale zabuni za mradi huo zitakapofunguliwa.
Mkurugenzi wa kampuni
hiyo,Allbles Shoo alipoulizwa kuhusiana na taarifa hizo mbali na kukiri kampuni
yake kupatiwa mkataba huo alisema kwamba
alishatoa kiasi cha sh,5 milioni kama ada ya mwezi Agosti mwaka huu.
Hatahivyo,alipoiulizwa
ya kuwa iweje apatiwe mkataba huo ihali muda wake ulimalizika mwaka jana
alisisitiza kwamba yeye alifuatwa na watumishi wa jiji hilo ambao walimpatia
mkataba na risitiza za malipo baada ya kuwalipa kiasi hicho.
Kaimu mkurugenzi wa
jiji la Arusha ambaye pia ni mhandisi mkuu wa jiji hilo,Lamsy alipotafutwa
alisema kuwa kulitokea makosa kwa wakala aliyeidhinishwa na jiji hilo kukusanya
ushuru wa makampuni mbalimbali yanayofanywa kazi na jiji hilo.
Lamsy,alimtaja wakala
wa Robert Advertisment kwamba ndiye aliyempelekea mkataba kampuni hiyo kimakosa
na kudai kwamba suala hilo linashughulikiwa ndani ya vikao vyao hadi sasa.