HUYU NDIE REDDS MISS PHOTOGENIC 2013






Mlimbwende Happiness Watimanywa (19) jana aliibuka kidedea kati ya walimbwende wenzake 30 na kutwaa taji la Redds Miss Photogenic 2013 na kupata nafasi ya kwanza kabisa kuingia Nusu Fainali ya mashindano hayo. Shindano hilo ni moja kati ya mataji matano ambayo yanashindaniwa na warembo hao ambapo washindi wake wanapata tiketi ya kuingia Nusu Fainali ya shindano hilo litakalo fanyika baadae mwezi ujao. Miongoni mwa mataji hayo ni Miss Tanzania Photogenic, Miss Tanzania Top Model, Miss Tanzania Personality, Miss Tanzania Sports Lady na Miss Tanzania Talent.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Lino International Agency, waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga 'Uncle' amesema jopo la majaji watatu ambao ni wapiga picha na wanahabari wazoefu wa masuala ya urembo Tanzania watakaa na kuchagua mshindi huyo kupitia picha mbalimbali za warembo hao.

Taji la Redd's Miss Tanzania Photogenic linashikiliwa na Mrembo Lucy Stephano aliyelitwaa mwaka 2012.

Mrembo huyo ambaye pia anashikilia taji la Miss Dodoma 2013 na Miss Kanda ya Kati 2013, ana digrii ya Biashara aliyoipata kupitia chuo cha Strathclyde University cha UK na aliwahi kuwa wa kwanza na kuongoza nchi zipatazo 150 katika somo la Accounts kwa shule zinazofanya mtandao wa IGCSE, Happiness alikuwa akisoma katika shule ya Saint Constantines International School ya Arusha. Alivumbuliwa na kipindi maarufu cha wanafunzi SKONGA kinachooneshwa kupitia televisheni ya EATV na kuwa mfano wa kuigwa kwa wanafunzi wengi nchini Tanzania na kwingineko.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post