Meneja wa Azania Bank tawi la Mbauda akimalizia hatua katika mbio za
Safari marathon,mshiriki huyu ndiye pekee alikuwa mwenye umri mkubwa
kwa upande wa changamoto za shirika .Alitumia dakika 40 kuhitimisha
mbio zake na kuzawadiwa mapumziko ya siku mbili katika hotel ya New
arusha hotel na waandaaji wa Safari marathon.
Afisa Masoko kanda ya kaskazini Bhoke Jackson akimalizia hatua za
mwisho katika mbio za Safari marathon zilizo fanyika jijini Arusha.
Maafisa wa benki ya Azania walioibuka vinara dhidi ya wenzao katika
mbio za kasi zaidi kwa jinsi ya kiume waliopo Benki ya Azania, kulia
ni mshindi wa kwanza Mohamed Goagoa,mshindi wa pili Jumanne Lucawa na
mwingine ni Afisa masoko tawi la Mbauda Salim Msangi.
Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi Hajira Mmambe akimalizia kukimbia
wakati wa mbio za Safari marathon zilizo fanyika jijini Arusha.
Wafanyakazi wa Benki ya Azania wakiwa katika picha ya pamoja nyuma ya
banda lao.
Meneja wa matawi ya benki ya Azania kanda ya kaskazini,kutoka shoto ni
Everist Mhogosi(meneja tawi laMbauda),Hajira Mmambe(meneja tawi la
Moshi) na Leonird Maliwa meneja tawi la Arusha city.
Wafanyakazi
wa Benki ya Azania wakijipongeza kwa msosi mara baada ya
kuhitimishwa kwa mbio za Safari marathon zilizofanyika jijini
Arusha.