LOWASA APATA UCHIFU UNYANYAMBE TABORA

Burudani mbali mbali.

Mh. Lowassa asimikwa kuwa Chifu wa Unyanyembe Mkoani Tabora leo,pia aweka jiwe la msingi Mnara wa kumuenzi Mtemi Isike Mwanakiyungi


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Machifu mbali mbali kutoka sehemu tofauti tofauti hapa nchini,wakati akiwasili kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mtemi Isike Mwanakiyungi wa Kabila la Unyamwezi aliefariki Miaka 124 iliyopita.Sherehe hizo zimefanyika leo kwenye Kijiji cha Itetemya,Mkoani Tabora.Kushoto ni Chifu Mkuu wa Unyanyembe,Chifu Msagata Fundikira
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akifurahia jambo na Mjukuu kutoka katika Ukoo wa Fundikira.Kushoto ni Chifu Mkuu wa Unyanyembe,Chifu Msagata Fundikira.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiangalia Ngoma za Asili ya Kabila la Unyamwezi waliokuwa wakitoa Burudani kwenye Sherehe hizo.
Mmoja wa Machifu wa Unyanyembe akimkabidhi Zawadi ya Asali,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akionyeshwa moja ya kibuyu cha Tambiko la Kabila la Unyamwezi.
Chifu Mkuu wa Unyanyembe,Chifu Msagata Fundikira akifanya tambiko muda mfupi kabla ya kumtawaza kuwa Mmoja wa Machifu wa Unyanyembe.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) akisikiliza kwa makini Wasifu wa Marehemu,Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki Miaka 124 iliyopita.Wasifu huo Ulisomwa na Bw. Richard Mchembe.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa pamoja na Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe,Chifu Msagata Fundikira wakishirikiana kuweka jiwe la msingi katika eneo litakalojengwa Mnara wa kumuenzi Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki Miaka 124 iliyopita.Sherehe hizo zimefanyika jana kwenye Kijiji cha Itetemya,Mkoani Tabora.
 Unyenyembe,Chifu Msagata Fundikira.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini,Mh. Ismail Aden Rage pamoja na Mbunge wa Jimbo la Sikonge,Mh. Said Mkumba waliokuwepo kwenye Sherehe hizo.
Sehemu itakayojengwa mnara huo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akivishwa vazi maalum la Kichifu pamoja na kukabidhiwa Mkuki na Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe,Chifu Msagata Fundikira ikiwa ni ishara ya kumsimika kuwa Chifu wa Kabila hilo,wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki Miaka 124 iliyopita.Sherehe hizo zimefanyika jana kwenye Kijiji cha Itetemya,Mkoani Tabora.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikabidhiwa cheti.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na Machifu.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa pamoja na Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe,Chifu Msagata Fundikira wakiwa kwenye picha ya pamoja na Machifu kutoka mikoa mbali mbali hapa nchini walioshiriki kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki Miaka 124 iliyopita.Sherehe hizo zimefanyika jana kwenye Kijiji cha Itetemya,Mkoani Tabora.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post