Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa kikundi cha Neema Womans Power Bi.Maryam Dedes kuelekea kwenye chumba cha mikutano katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kabla ya kukabidhi msaada wa Magodoro kwenye Hospitali hiyo.
Mkurugenzi wa Wauguzi Hospitali ya Muhimbili Bi. Agnes Jonathan Mtawa akizungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili katika uotaji huduma kwa wananchi mbele ya mgeni rasmi Mstahihiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa katika hafla fupi ya kukabidhi Magodoro 50 kwa Hospitali hiyo.
Katibu wa Neema Womans Power Mgeni Ottow akisoma risala yao mbele ya mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi Magodoro 50 kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akikabidhi rasmi Magodoro 50 kwa Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akimshukuru Mwenyekiti wa kikundi cha Neema Womans Power Bi.Maryam Dedes (mwenye hijabu nyekundu) mara baada ya kukabidhi Magodoro hayo.
Mwenyekiti wa kikundi cha Neema Womans Power Bi.Maryam Dedes katika picha ya pamoja na Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na Wakinamama wa Kikundi cha Neema Womans Power.
Na. Mwandishi wetu.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala MH.JERRY SILAA amekabidhi magodoro 50 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupitia kikundi cha wakimama "NEEMA WOMANS POWER".
Neema Womens Power ni kikundi cha wakina mama kilichoanzishwa mwaka 2005 kwa kuanza na Madrasa mbili ya akinamama na wasichana akiwa na wanafunzi 18 tu. Madrasa hizo zipo Kinondoni na Buguruni chini ya Mwenyekiti wa kikundi hicho Bi.Maryam Dedes. Jumuiya hii pamoja na kuwa na Elimu ya dini, husaidia jamii kwa michango mbalimbali ikiwemo kulipia ada za shule kwa wanafunzi wasiokuwa na uwezo, kusaidia Walemavu na Wajane pamoja na familia duni.
Katika hafla hiyo fupi Mgeni rasmi Mh. Jerry Silaa ametoa wito kwa wadau mbalimbali kuweza kujitoa kwa kusaidia jamii kwani mzigo uliopo kwa Serikali peke yake haiwezi, na ukizingatia ya kwamba hakuna mtu asiyeijua Hospitali kama si Muhimbili basi Amana, Temeke au Mwananyamala na Hospitali nyingine nyingi zinahitaji msaada vifaa mbalimbali na endapo kila mwananchi angeweza kuchangia japo kifaa kimoja sasa tungekuwa mbali sana na inawezekana kabisa tusingekuwa na matatizo sugu katika Hospitali zetu.
Mh.Jerry ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha huduma zinaboreshwa ndani ya Halmashauri yake na anayesifika kwa uchapakazi wake na umakini aliwashukuru kwa dhati kabisa uongozi wa Neema Womans Power pamoja na wanachama wao kwa kuliona tatizo hilo na kwa uwezo walionao leo hii wameweza kutoa magodoro hayo 50 na kuwaasa waendelee kujitoa zaidi na wasife moyo maana kazi ya jamii haina malipo zaidi ya fadhira mbele za Mungu.
Hafla hiyo fupi ya kukabidhi Magodoro imehudhuriwa na Bi.Maryam Dedes ambaye ni Mwenyekiti wa kikundi hicho, Agnes Jonathan Mtawa- Mkurugenzi wa Wauguzi Hospitali ya Muhimbili, Mgeni Ottow Katibu wa Neema Womans Power pamoja na Khadija Mwita Makamu mwenyekiti na wajumbe wao 30 na Uongozi wa Hospitali ya muhimbili.