MAPAMA
jana Dar es salaam, Waziri wa nchi ofisi ya waziri Mkuu sera na uratibu
wa shughuli za Bunge Wiliam Lukuvi alisema Serikali inafuatilia kwa
karibu kesi zinazowahusisha Watanzania waliopo nje ya nchi wanaotuhumiwa na biashara ya dawa za kulevya wakiwemo wanamichezo na wasanii mbalimbali.
Alisema ilikuthibitisha hali hiyo timu ya watendaji imetumwa nchini
Afrika kusini hivi karibu ili kukutana na kina Masogange kujua undani wa
kesi yao na imethibitika kuhusika kweli na tuhuma hizo ambapo
inasadikiwa jana kesi yao imesomwa rasmi na kusubiri hatua zaidi za
kisheria.
Akizungumzia taarifa za kukamatwa kwa mwanamichezo Kaniki na Matumla,
Lukuvi alisema taarifa hizo zitatolewa ufafanuzi zaidi na Serikali baada
ya kupokea taarifa za kiofisi kutoka nchini Ethiopia.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha kupambana na kudhibiti na dawa za
kulevya Godfrey Nzoa alisema kati ya timu waliokwenda Afrika kusini ni
pamoja na yeye mwenyewe ambaye alifanikiwa kukaa kwa karibu na wafungwa
hao akiwemo Masogange na kubaini kuna siri nzito mgongoni mwa Mwasogange
hivyo inahitaji uchunguzi ili mkono wa sheria uweze kuwagusa wote
wanaohusika na kutumia wasanii katika janga hilo.
“Ni kweli masogange na wenzie wamekamatwa na dawa aina za Ephedrine
ambazo ndio zinazotengeneza dawa za kulevya na zinaruhusiwa kuingia nchi
yeyote kwa kibali malaum kwani pia zinahusika kutengeneza dawa za kifua
na timu iliyotumwa na Serikali imeweza kuzungumza nao lakini
haimaanisha kwenda kwetu gerezani tunawatetea au tutawasaidia hapana
kwakua hawakutumwa kufanya baisahara hiyo haramu ila tunajaribu kuwa
karibu ili kuona wanapata haki zao na kuweza kubaini waliopo nyuma yao
na kweli tumefanikiwa mnyororo ni mrefu tunaendelea na uchunguzi ili
kujua wafadhili na mabosi zao tunawatiaje mikononi”alisema
Aliongeza kuwa ameshangazwa na kipato kidogo wanachopata wasanii hao
akiwemo Masogange ambapo Afande Nzoa hakutaka kukiweka hadharani ili
kupisha uchunguzi zaidi huku akiongeza kuwa kufuatia sheri iliyopo
wasanii hao kesi zao zitafanyika Afrika kusini kwakua ndiko
walikokamatiwa na endapo kuna mkataba wa ubadilishana wafungwa Serikali
itaangalia njia ya kuwasaidia ili watumikie vifungo vyao nchini
Na jumamtanda
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia