Ticker

6/recent/ticker-posts

WEZI WA MAJI MJINI MOSHI WAKAMATWA NA MUWSA

Kazi imefanyika usiku mkubwa chini ya usimamizi wa askari polisi.
Sehemu ya mauongio ya maji katika njia kuu ya maji iliyopita ndani ya eneo hilo.
Ofisa uhusiano wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi,Dorah Killo akiangalia moja ya tanki la ardhini ambalo limekuwa likitumika kuhifadhia maji ambayo yameunganishwa kwa wizi kwa ajili ya kunyweshea na kuogeshea Nguruwe.
Sehemu ambako hujuma ya maji imekuwa ikifanyika katika moja ya eneo la kufugia Nguruwe katika kata ya Korongoni.
Fundi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi.MUWSA akichimba eneo ambalo kuna bomba la maji lililounganishwa kwa wizi katika miuondo mbinu ya mamlaka hiyo.
Nguruwe zaidi ya 70 wanaofugwa katika eneo hilo ambao maji yaliyounganishwa kwa njia ya wizi yamekuwa yakitumika kuwaogesha na kunyweshea.Shoto ni ofisa uhusiano msaidizi wa MUWSA ,Florah Stanley.
Mafundi wakiendelea kufukua bomba lililounganishwa kwa wizi.
Baada ya kusimama muda mrefu baadhi ya watu waliokuwa wakishuhudio tukio hilo la kutafuta maungio ya maji walilazimika kunywa maji yale yale yaliyoungwa kwa wizi.
Sehemu ya mauongio ya maji katika njia kuu ya maji iliyopita ndani ya eneo hilo.
Baada ya kusimama muda mrefu baadhi ya watu waliokuwa wakishuhudio tukio hilo la kutafuta maungio ya maji walilazimika kunywa maji yale yale yaliyoungwa kwa wizi.


SIKU chache baada ya mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi (MUWSA) kubaini kufanyiwa hujuma ya wizi wa maji katika mitandao yake,mamlaka hiyo sasa imeanzisha operesheni isiyo na kikomo huku ikiwatumia askari polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia(FFU) kusaka wezi hao nyumba kwa nyumba.

Operesheni hiyo imeanza hivi karibuni katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi hususani yale yenye viwanda na maeneo yanayokaliwa na watu wa kipato cha juu ambayo yanatajwa kujihusisha na wizi wa maji kwa kujiunganishia kinyume cha sheria.

Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi,John Ndetiko alisema operesheni hiyo imeanza wakati huu ambao kuna upungufu mkubwa wa maji hivyo ufuatiliaji utafanyika katika eneo moja hadi jingine ili kuwabaini wezi wa maji.

“Zoezi hili litakuwa ni endelevu kabisa katika kipindi chote cha uhai wa mamlaka ya maji taka na maji safi mjini Moshi na tumeamua kuianza sasa kutokana na kuwepo kwa upungufu mkubwa wa maji katika maeneo mengi kwa hiyo tutafanya ufuatiliaji katika eneo moja baada ya na jingine ili kuwabaini wanaofanya hujuma hiyo na kuwapeleka kwenye vyombo vya sheria.”alisema Ndetiko.

Akizungumzia kwa nini wameamua kuwatumia askari polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia(FFU)Ofisa uhusiano wa mamlaka hiyo Dorah Kilo alisema sheria za mamlaka zinaruhusu maofisa wake kuingia sehemu yoyote kwa mtu anayetumia maji ama hatumii maji kwa lengo la kukagua miundo mbinu isifanyiwe hujuma.

Alisema kumekuwa na changamoto kubwa ya kiusalama kutokana na maeneo mengine watumiaji wa maji wamekuwa hawatoi ushirikiano kwa kufungua milango yao licha ya kujitambulisha kwao hali inayopelekea kutumia jeshi la polisi pamoja na viongozi wa mitaa husika.

“Mara nyingi tunatangulia sisi wenyewe katika eneo husika,tunakuja kirafiki tunazungumza ili kuweza kutambua matatizo yako na kasha kuchukuliwa hatua, lakini unapokuwa unaleta ugumu wa kutoa ushirikiano pale ndipo tunalazimika kuwaagiza askari polisi kuja kuongeza nguvu.”alisema Killo.

Alitoa wito kwa wakazi wa mji wa Moshi na maeneo mengine yanayosimamiwa na mamlaka hiyo kutoa taarifa za hujuma ya maji katika maeneo yao na kwamba atakayotoa taarifa sahihi ya wizi huo atazawadiwa na mamlaka hiyo kiasi cha fedha ambazo hata hivyo hakukitaja.

Post a Comment

0 Comments