SABABU ZINAZOSABABISHA WANAWEKE WENGI WASISHIKE MIMBA HIZI HAPA

Na Dk. Chale

MWANAMKE kutoshika mimba kumegawanyika katika makundi makubwa mawili. Kwanza ni hali iitwayo ‘primary Infertility’ ambapo mwanamke hana historia ya kupata ujauzito. Pili kuna hali iitwayo ‘Sekondari Infertility’, hapa mwanamke anayo historia kama alishawahi kupata ujauzito haijalishi kama alizaa au alitoa au iliharibika.

Matatizo ya kutoshika mimba kwa mwanamke kitaalamu tunaita ‘infertility’ au ugumba.

Kutoshika mimba kwa mwanamke husababishwa na mambo mengi ingawa tutakuja kuona vyanzo vikuu.

Maambukizi katika viungo vya uzazi, hali duni ya lishe na magonjwa sugu pia huathiri hali hii ya ugumba kwa mwanamke.



Chanzo cha matatizo ya ugumba kwa mwanamke

Vyanzo vya matatizo haya vinahusisha aina zote mbili za ugumba za ‘Primary’ na sekondari’. Kwanza…
Na Dk. Chale
MWANAMKE kutoshika mimba kumegawanyika katika makundi makubwa mawili. Kwanza ni hali iitwayo ‘primary Infertility’ ambapo mwanamke hana historia ya kupata ujauzito. Pili kuna hali iitwayo ‘Sekondari Infertility’, hapa mwanamke anayo historia kama alishawahi kupata ujauzito haijalishi kama alizaa au alitoa au iliharibika.
Matatizo ya kutoshika mimba kwa mwanamke kitaalamu tunaita ‘infertility’ au ugumba.
Kutoshika mimba kwa mwanamke husababishwa na mambo mengi ingawa tutakuja kuona vyanzo vikuu.
Maambukizi katika viungo vya uzazi, hali duni ya lishe na magonjwa sugu pia huathiri hali hii ya ugumba kwa mwanamke.

Chanzo cha matatizo ya ugumba kwa mwanamke
Vyanzo vya matatizo haya vinahusisha aina zote mbili za ugumba za ‘Primary’ na sekondari’. Kwanza kabisa ni chanzo kinachohusu upevushaji wa mayai ‘Ovulatory’. Tatizo hili huathiri wanawake kwa kiasi kikubwa ambapo mwanamke anapata siku zake kama kawaida lakini hapevushi mayai.
Hii husababishwa na matatizo katika mfumo wa homoni mwilini, tatizo linaweza kutokea lenyewe kutokana na mabadiliko ya mwilini au matumizi yanayohusiana na dawa za homoni kutumika kiholela au matumizi ya baadhi ya vyakula au vipodozi, tutakuja kuona.

Katika makala zijazo
Dalili za upevushaji wa mayai zipo nyingi, tutakuja kuziona hapo baadaye lakini kubwa ni kwa mwanamke kupata ute wa uzazi ambapo upo wa aina tatu.
Pia upevushaji tunaweza kuuona kwa kutumia vifaa maalumu ambavyo unatumia mwenyewe nyumbani kwa kupima mkojo siku unazohisi unaweza kupata mimba.
Tatizo lingine la chanzo cha ugumba ni kwenye mirija, mirija inaweza kuziba, kutanuka au kuweka usaha au maji. Maambukizi katika mirija au upasuaji wa mimba nje ya kizazi au kufunga kizazi.
Utoaji wa mimba, maambukizi ya mara kwa mara ukeni husababisha athari katika kizazi na mirija. Matatizo ya mirija husababisha ugumba kwa kiasi kikubwa ambacho ni kati ya asilimia 15 hadi 40 kwa wanawake ambacho ni kiwango kikubwa kuliko matatizo mengine.
Mwanamke pia anaweza kuwa na kasoro katika tabaka la ndani la kizazi ambapo linatoka kwa nje badala kuwa ndani. Hali hii kitaalam inaitwa ‘Endometriosis’. Siyo tatizo linalojitokeza kwa ukubwa sana lakini linaathiri baadhi ya wanawake.
Mwanamke mwenye tatizo hili hulalamika maumivu chini ya tumbo na huwa makali wakati wa hedhi na kusababisha damu ya hedhi kutoka kidogokidogo, mwanamke hupoteza uwezo wa kushika mimba.
Matatizo ya mwanaume kushindwa kufanya tendo la ndoa, anamaliza lakini manii hazitoki pia husababisha ugumba kwa mwanaume ambao humuathiri mwanamke. Mwanaume pia anaweza kufanya tendo la ndoa vizuri, anatoa manii lakini mbegu hakuna, hili pia ni tatizo kubwa.
Mwanaume anaweza kupata tatizo la uzazi hata kama anayo historia ya kumpa mwanamke mimba au kuwa na watoto kwa hiyo ni vema naye akafanyiwa  uchunguzi endapo wanatafuta mtoto au ujauzito kwa mwaka mmoja bila ya mafanikio.
Ugumba pia unaweza kutokea na baada ya uchunguzi wa kina inaonekana mume hana tatizo wala mke hana tatizo, hali hii inaitwa kitaalamu ‘Unexplained Inferlity.  Kwa hiyo, ni vema uchunguzi wa kina ufanyike. Tatizo hili tutakuja kuliona katika makala zijazo.

Uchunguzi
Matatizo ya ugumba ni makubwa na huumiza vichwa vya watu wanaotafuta ujauzito. Tumeona sababu kuu za ugumba lakini mambo mengine  yanayohusiana na lishe na magonjwa sugu yanayoathiri uzazi. Tutakuja kuzungumzia.
Uchunguzi hufanyika kwa madaktari wa magonjwa ya kinamama na matatizo ya uzazi katika hospitali za mikoa na wilaya. Vipimo mbalimbali hufanyika kama damu kuangalia viwango vya homoni, ultrasound na mirija uzazi.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post