Mnyama huyu anajulikana kama Statunga anapatikana katika hifadhi ya Lubondo hifadhi ambayo ipo katika ziwa victoria na mnyama huyu katika mbuga za Tanzania anapatika Lubondo
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya hapa nchini wakiwa wanasikiliza maelezo ya mawe makubwa yaliyopo katika hifadhi saa nane iliyopo katika ziwa victoria mawe hayo kwa mujibu wa muhifadhi wa hifadhi ya saa nane Rukia anasema kuwa hapo ndipo wahindi wanapo kwenda kufanyia mila zao kwa mkoa wa mwanza
waandishi waandamizi waliouthuria katika ziara ya kutembelea mbuga mbalimbali hapa walikuwa katika hifadhi ya taifa ya gombe iliyoko katika kisiwa kimoja wapo kilichopo ziwa victoria mkoani mwanza wakwanza kushoto ni Unos Masanja wa Stax TV akifuatiwa na woinde shizza wa gazeti la Nipashe anayemfuata kushoto ni ben wa TBC huku wa kwanza kulia ni Gwandu wapili kulia ni Lilian Johel wa gazeti la uhuru
Baadhi ya waandishi wa habari wakipata msosi mara baada ya kutoka katika hifadhi ya Lubondo katika mgahawa ujulikanao kama kwa mama Nasoro uliopo nje kidogo wa mji wa Mwanza katika msafara huu mpiganaji Mussa Juma ndiye alikuwa mwenyekiti wa kikosi hichi au kwa luga ingine msafara huu
Wananchi wakivuka katika kivuko cha mto madagarasi ulioko mkoani Kigoma
Kwa hapa nchini Tanzania mbuga inayoongoza kwa kuwa na viboko wengi ni Mbuga ya Katavi iliyoko mkoani Rukwa hapa ni viboko wakiwa wanakula raha ndani ya maji katika ziwa katavi lililopo mkoani Rukwa mbuga hii inayoongoza kwa kuwa na viboko wengi hadi sasa kuna zaidi ya viboko 3000
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia