Kikosi
cha Taswa Fc kutoka Jijini Dar es Salaam kilichoshiriki mechi
mbalimbali kwa mtindo wa ligi katika Bonanza la Wanahabari na Wadau wa
Habari Jijini Arusha. Bonanza hilo limeandaliwa na Taswa Arusha kwa
udhamini wa TBL, TANAPA, Mega Trade, Coca Cola Zero, Pepsi.
Kwa
mujibu wa Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo mkoani
Arusha, Bw Musa Juma jumla ya timu 12 zilitarajiwa kushiriki, kukiwa na
michezo mingine kama kufukuza kuku,kukimbia na magunia,mpira wa miguu
,mpira wa pete, bila kusahau burudani ya muziki kutoka kwa bendi
iliyoalikwa na dj
Baadhi
ya timu zilizo shiriki katika tamasha hili la nane kuandaliwa na Taswa
Arusha, ni pamoja na Taswa Fc ya Jijini Dar es Salaamu ambapo, Taswa
Arusha ambao ni wenyeji wa bonanza.
Wengine ni timu ya ORS Fm ya
Manyara, timu ya Sunrise fm, Radio five, AJTC, pamoja na timu ya
TBLambao ni miongoni mwa wadhamini.
Winga wa Taswa FC ya Dar akipiga mpira wa adhabu ndogo kuelekea langoni mwa timu ya Redio Five ya Jijini Arusha
Timu
za AJTC (wenye njano) wakiwa katika ukaguzi na timu ya Arusha One
redio. Arusha one waliibuka washindi kwa 2-1 katika mechi hii.
Wachezaji
wa Arusha One wakipatiwa maelekezo na waratibu wa Bonanza kabla ya
mechi kuanza katika kusisitiza mchezo wa upendo na amani.
Timu
ya ORS Fm toka Manyara (wenye njano) pamoja na timu ya Sunrise Fm ya
Jijini Arusha kabla ya mpambano wao ulioisha kwa Sunrise kuibuka
washindi kwa goli 2 dhidi ya 1 la ORS.
Katibu wa Taswa Arusha, Mussa Juma (mwenye kofia) akichambua majina ya baadhi ya wachezaji na waratibu wenzake wa Bonanza hilo.