TAASISI YA FEDHA TIB YAPANDISHWA HADHI NA KUWA BENKI YA MAENDELEO

01
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro (kulika) akikata utepe kuzindua ofisi za Makao Makuu ya Benki ya Maendelea Tanzania (TIB) ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Tawi la benki hiyo Mkoa wa Mbeya iliyofanyika jijini Mbeya jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa TIB, Peter Noni na Mwenyekiti wa Bodi ya TIB, Prof. William Lyakurwa.
02
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo Tanzania (TIB), Prof. William Lyakurwa (kushoto), akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa ofisi za Makao Makuu ya TIB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Tawi la benki hiyo Mkoa wa Mbeya iliyofanyika jijini Mbeya. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro na Mkurugenzi Mwezeshaji wa TIB, Peter Noni.
03
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro (katikati) akijaza fomu ili kufunguliwa akaunti ya Benki ya Maendeleo Tanzania (TIB) Tawi la Mbeya, katika hafla ya ufunguzi wa ofisi za Makao Makuu ya TIB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini pamoja na tawi hilo Mkoa wa Mbeya iliyofanyika jijini humo. wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa TIB, Peter Noni na anayeongea naye ni Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi.
.ilianzishwa mwaka 1970 ina takribani miaka 40 kwenye huduma za kifedha
.sasa kuwekeza kwenye miundombinu ya reli, mawasiliano na barabara
.Benki ya wanyonge, mafanikio kichelee, wakulima nao kunufaika
Na Damas Makangale, Moblog
Baada ya kujiendesha Kwa faida Kwa takribani muongo mmoja, Benki ya Maendeleo Tanzania (TIB) iliyoanzishwa mwaka 1970 Kama Taasisi ya Maendeleo ya fedha, Development Finance Institution (DFI), TIB inakusudia kuanza kuwekeza katika miradi mikubwa yenye kuleta matokeo makubwa na kuendana na kauli mbiu mpya ya Serikali “Matokeo Makubwa sasa” (Big Results Now).
Baada ya kufanya kazi Kama taasisi ya maendeleo ya fedha Kwa miaka 25, TIB ilikuja kubadilishwa na kuwa benki ya uwekezaji (Tanzania Investment Bank) ili kuongeza uwezo wake wa kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya soko hapa nchini.
TIB lengo lake kuu ni kutoa Fedha na huduma za uwekezaji na maendeleo katika Nyanja mbalimbali kama vile kilimo kupitia dirisha lake maalum la kukopesha wakulima wadogo wadogo (Special Agriculture Window), mikopo kwa wafanyabiashara na watu wa kipato cha chini ili kuweza kuinua maisha yao na kuondokana na umaskini.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post