Ticker

6/recent/ticker-posts

NGORONGORO CONSERVATION YATOA MSAADA WA CHAKULA KWA WANANCHI WAISHIO NDANI YA ENEO LA HIFADHI

Wakazi wa eneo la mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro wakipokea chakula cha msaada kutoka kwa uongozi wa Ngorongoro Conservation Are Authority (NCAA) ikiwa ni agizo kutoka kwa waziri mkuu mizengo pinda.

Tani 7000 zimegawiwa kwa familia 20,000 za jamii ya wamasai wanaoishi katika hifadhi hiyo. Idadi ya watu ndani ya NCAA kwa sasa ni zaidi ya 87,000 na wote wakiwa na mahitaji makubwa ya chakula kwani hawaruhusiwi kulima ndani ya eneo la NCAA.

Hivi karibuni wamasai hao wamejukuta wakikumbwa na baa la njaa baada ya ukame ulioathirini eneo lao kwa miaka mitatu mfululizo kuteketeza mifigo ambayo hasa ndiyo tegemeo lao la maisha.

Ugawaji wa chakula umeanza katika kata ya Olbalbal na utaendelea kwenye maeneo mengine huku NCAA ikijiandaa kununua tani zingine 29,000 za mahindi kutoka wilayani Karatu kwa ajili ya kuongeza mgawo huo wa chakula.

Post a Comment

0 Comments