RAY C AINGIA MZIGONI KUFANYA MAMBO



Haya wale wenye kiu na ujio mpya wa Ray C mnaweza kuanza kuandaa makoo yenu sababu chakula kimeshawekwa jikoni na muda si mrefu mnaweza kukaribishwa mezani.

Ray C ameshea picha kadhaa akiwa studio na wadau mbalimbali akiwemo Bab Tale na Said Fella, na kama haitoshi ameweka mashairi ya wimbo wake ambao unaonekana ndio aliokuwa akiurekodi wakati anapiga picha hiyo na kuandika “Mashairi ya my new song…,its a very beautiful song…am sooooooo happy..Thank you Lord”.
Ray C lyrics
Unaweza kuyapitia na kuanza kutengeneza taswira ya kile kinachokuja kutoka kwa Rehema Chalamila amabaye anasubiriwa kama nguo ya Christmas au Idd kwa watoto.

Pia Ray C amesema album yake inakuja hivi karibuni

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post