Baadhi ya waombolezaji waliofika kwenye msiba wa Mzee Arnold Nkhoma wakisaini kitabu cha maombelezo nyumbani kwa mmoja wa mabinti wa marehemu Prof. Alice Wamunza Nkhoma.
Baadhi ya waombolezaji wakimfariji mmoja watoto wa marehemu Bi. Agnes Nkhoma Darch (katikati).
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa mtoto wa marehemu Prof. Alice Wamunza Nkhoma, Changanyikeni - Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Roy Ledama (kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya waombolezaji.
Familia ya Marehemu Mzee Arnold Nkhoma pamoja na waombolezaji wakipata chakula cha mchana kabla ya kutoa heshima za mwisho.
Gari lilibeba mwili wa Marehemu Mzee Arnold Wifred Nkhoma likiwasili nyumbani kwa binti yake Changanyikeni, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Wajukuu wa marehemu wakiwa wamebeba Jeneza la Babu yao kuliingiza ndani tayari kwa heshima za mwisho kabla ya kuelekea Kanisani kwa Ibada.
Mwili wa Mzee Arnold Wifred Nkhoma tayari kwa kutoa heshima za mwisho.
Familia ya karibu ya marehemu.
Kushoto ni mabinti wawili wa Marehemu wakiwa na ndugu zao wakaribu kwenye majonzi mazito.
Vitukuu wa marehemu mzee Arnold Nkhoma.
Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho.
Mtoto wa Marehemu Prof. Alice Wamunza Nkhoma akitoa heshima za mwisho kwa baba yake mpendwa Mzee Arnold Nkhoma.
Mtoto wa marehemu Bi. Agnes Nkhoma Darch akitoa heshima kwa baba yake.
Mjukuu mkubwa wa marehemu Bi. Usia Nkhoma Ledama akitoa heshima za mwisho kwa babu yake.
Vilio na simanzi vilitawala.
Ndugu wa karibu wa marehemu wakiendelea kutoa heshima za mwisho.
Mama Usia na mjukuu wake Vanessa Roy Ledama wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu.
Mjukuu wa marehemu Bi. Sawiche Wamunza Nkhoma akitoa heshima za mwisho kwa babu yake.