MAISHA
katika uso wa dunia ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Kalenga,
Dk William Mgimwa yamehitimishwa jana kijijini kwake Magunga wilayani Iringa
mkoani Iringa.
Rais
Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda waliongoza watu wanaokadiriwa kuwa
10,000 kuupumzisha mwili wa Dk Mgimwa katika nyumba yake ya milele.
Pamoja
na Rais na Waziri Mkuu, mawaziri mbalimbali, wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu wa
wilaya, watendaji wa wizara, na viongozi wa CCM na vyama vya upinzani
walihudhuria mazishi hayo.
Rais Kikwete na wasaidi wake |
Akiendesha
ibada ya kumuombea marehemu, Msaidizi wa Makamu wa Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki
Songea, Julius Kangalawe aliomba Mungu awajalie na awape maisha marefu
wanasiasa wanaohangaikia masikini.
“Siku
hizi hakuna udugu, wenye nacho wanataka kuendelea kuwa nacho, watu wanaogopana,
udugu umechakachuliwa na masikini wanaendelea kuwa masikini,” alisema.
Tofauti
na viongozi wengi, alimsifu Dk Mgimwa kwa kuwa mnyenyekevu, mpenda watu na
aliyetumia akili zake nyingi alizokuwa nazo kwa maendeleo ya watu.
“Umati
huu mkubwa wa watu unadhihirisha jinsi Dk Mgimwa alivyokonga nyoyo za watu;inaonesha
jinsi alivyokuwa mpenda haki, leo amepumzishwa katika nyumba yake hii, kesho
hatujui nani atamfuata, lakini watakaomfuata wapo hapa hapa,” alisema.
Alimuomba
Mungu awajalie watanzania wawe na siasa bora inayojali masikini kwa kuwa hiyo
ndiyo njia ya kuwafananisha binadamu.
“Leo
hii wanasiasa wanaingia katika ofisi zao
baada ya kuomba Mungu kwa kutumia vitabu vitakatifu, lakini wengi wao ni
waongo; wanatumia maandiko matakatifu kufanya udanganyifu, wakishakula kiapo,
na vitabu vya Mungu wanatupa,” alisema.
Alisema
pamoja na kiu kubwa waliyonayo watanzania ya kupata Katiba mpya, haiwezi
kuwasaidia kwasababu bila Mungu hakuna linalowezekana.
“Hata
katiba hiyo iwe nzuri kiasi gani, majambazi wataendelea kuwa majambazi,
mafisadi vivyo hivyo na masikini wataendelea kudhulumia haki zao, kwasababu
hakuna upendo wa Mungu,” alisema.
Alisema
Katiba pekee inayoweza kumaliza matatizo ya watanzania ni zile sheria
zilizoandikwa na Mwenyezi Mungu kwani ndizo zenye uwezo wa kubadili maisha.
Akitoa
salamu za serikali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema afya ya Dk Mgimwa ilianza
kuteteleka alipokuwa kikazi Marekeni mwishoni mwa mwaka jana.
“Serikali
iliamua kumpeleka Afrika Kusini kwa matibabu, hata hivyo Mungu alimpenda zaidi
na akayachukua maisha yake,” alisema.
Alisema
Dk Mgimwa alikuwa mchapa kazi aliyeonesha muelekeo wa kuituliza serikali katika
nafasi nyeti ya Waziri wa fedha.
“Serikalini
tulianza kutulia, tukiamini wizara imepata mtu; kazi tuliyonayo ni kuenzi tunu
alizokuwa nazo. Alikuwa mchapa kazi mwenye akili nyingi,” alisema.
Mwakilishi
wa kambi ya Upinzani Bungeni, Mchungaji Peter Msigwa (MB) alisema taifa
lilikuwa linamuhitaji Dk Mgimwa kwani alionesha tofauti kubwa na wazee wengine
kwa kujali maendeleo ya watu.
“Alikuwa
makini bungeni, aliacha itikadi za vyama alipokuwa akitekeleza majukumu yake,
na mara kadhaa alikuwa akichukua hoja za wapinzani na kuzifanyia kazi,”
Mchungaji Msigwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini alisema.
Alisema
binadamu hawajaumbwa ili kuleta matatizo kwa wengine na ndio maana thamani ya
utu wao huhesabiwa kwa haki wanayotenda kama alivyokuwa Dk Mgimwa.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk Christine Ishengoma alimkumba Dk Mgimwa kwa uchapi
kazi wake huku akiwasilisha rambirambi ya Sh Milioni 5 kwa familia ya marehemu.
Akitoa
shukrani za familia, mtoto wa Dk Mgimwa, Godfrey Mgimwa alizitaja kazi nyingi
zilizkuwa zikitekelezwa na baba yake katika jimbo lake la Kalenga na kuiomba
serikali kuziendeleza.
Kazi
hizo ni pamoja na kusomesha watoto yatima, ujenzi wa mabweni katika shule za
sekondari, ujenzi wa miundombinu na mawasiliano, misaada kwa vikundi vya
ujasriamali, na mkazo katika huduma za jamii ikiwemo afya, kilimo, na maji.
Alisema
siku kumi kabla ya kifo cha baba yake, alimwambia ameandaa mabati 120 anayotaka
kuyagawa katika maeneo mbalimbali jimboni mwaka kwa lengo la kusukuma
maendeleo.
Alimpongeza
Rais Kikwete kwa upendo na ushirikiano aliotoa kwa familia yao katika kipindi
chote ambacho baba yao alikuwa mgonjwa hadi kifo chake.
“Rais
alionesha uzalendo na upendo wa hali ya juu kwani alimtembelea baba mara mbili
akiwa amelazwa hospitalini,” alisema.
wawakilishi taasisi za fedha |
wakuu wa wilaya na mikoa |
Joseph Mungai akiwakilisha wazee |
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia