Kijana Salum Nyangumwe (17) mshindi wa pili aliyeimba wimbo wa My Number One wa Msanii Nasib Abdul a.k.a Diamond wakati wa fainali za kusaka kipaji cha SUPA STAA wa watoto na vijana! la ”MO Kids Got Talent 2013" lililofanyika mwishoni mwa Juma kwenye Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Na.Mwandishi wetu.
Mtoto Moureen Julius(12), amejinyakulia kitita cha shilingi Milioni tano katika fainali za Shindano la “MO KIDS GOT TALENT 2013” lililofanyika kwenye hoteli ya Ledger Plaza Bahari beach lililoanza tarehe 25 hadi tarehe 28 mwezi huu ambapo fainali zilifanyika.
Shindano hilo lilijumuisha watoto zaidi ya mia mbili ambapo kila mmoja alijipatia nafasi ya kuonesha kipaji chake vikiwemo kuogelea, kuimba, kucheza, karate na vingine vingi.
Watoto 15 walichuana katika nusu fainali na kuchujwa hadi kufikia watoto watano na mwisho wa siku kupatikana SUPA STAA Moureen Julius aliyewafunika wenzake kwa kipaji alichonacho.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa mshindi wa kwanza aliyejinyakulia kitita cha sh.millioni tano, Mtoto Moureen Julius alisema pesa hizo alizoshinda atazitumia kwa kulipia ada na vifaa vingine vya shule.
Shindano hili la "MO KIDS GOT TALENT 2013" liliandaliwa na Frost Africa na kudhaminiwa na Mohammed Enterprises Tanzania Ltd. (MeTL) Group.
Supa Staa wa Shindano la "MO Kids Got Talent 2013" Moureen Julius (12) akionyesha kipaji chake cha kucheza kwenye fainali za shindano hilo.
Pichani juu na chini washiriki wa shindano la "MO Kids Got Talent 2013" wakiendelea kuonyesha vipaji vyao wakati wa fainali za shindano hilo.
Mtoto mwenye kipaji cha kuimba na kucheza.
Jaji Hidaya Njaidi akitoa maoni yake kwa washiriki (hawapo pichani) waliokuwa wakichuana kuwani Shilingi Milioni 5 za Kitanzania zilizotolewa zawadi na Kampuni ya MeTL Group.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Frost Africa, Bw. Peter Sekasiko ambao ndio waandaji wa mashindano hayo na Meneja Masoko Msaidizi wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali (kulia) wakifuatilia kwa umakini mashindano hayo yaliyomalizika mwishoni mwa Juma.
Jaji Mkuu wa shindano la "MO Kids Got Talent 2013" Salma Mziray akitoa maoni yake kwa washiriki waliofanikiwa kuingia tano bora.
Pichani Juu na chini ni baadhi ya washiriki waliofanikiw kuingia tano bora wakionyesha manjonjo yao kwa mara nyingine tena kabla ya kutajwa mshindi wa shilingi Milioni tano kutoka Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd. MeTL Group lilifanyika mwishoni mwa Juma kwenye Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar.
Jaji Kiongozi wa shindano la "MO Kids Got Talent 2013" akiteta jambo na Raisi wa wanafunzi, Allan Lucky a.k.a SKONGA kabla ya kutangaza mshindi.
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer na Afisa Mtendaji Mkuu wa Frost Africa, Bw. Peter Sekasiko wakionekana kufurahishwa na vipaji vya watoto hao.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Frost Africa, Bw. Peter Sekasiko, akitoa nasaha kwa washiriki walioingia tano bora ambapo amewata wazazi kuhakikisha wanaendeleza vipaji vya watoto.
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer, akiwapongeza vijana walioingia tano bora.
Tano Bora wakiwa na matumbo joto.
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer, akitoa nasaha zake ambapo amesema mashindano haya yatakuwa yakifanyika kila mwaka nchini lengo ni kuibua vipaji vya watoto na vijana.
Mshindi wa tano Gloria Collin (10), akipokea maboksi ya zawadi zilizotolewa na kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd (MeTL) kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Frost Africa, Bw. Peter Sekasiko ambao ndio waandaji wa mashindano hayo.
Mshindi wa nne Lisa Deogratius (17) naye alipkeza zawadi mbalimbali kutoka kampuni ya MeTL.
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer, akiwausia washiriki ambao mmoja kati ya hao ataibuka mshindi wa kitita cha shilingi milioni tano kutoka MeTL Group.
Jaji Kiongozi wa shindano la "MO Kids Got Talent 2013" Salma Mziray akitoa shukrani kwa kampuni ya MeTL kwa kuweza kuibua vipaji vya watoto na vijana.
Na mshindi niiiiiiiiiiiii.....!!!! Raisi wa wanafunzi, Allan Lucky a.k.a SKONGA akitangaza mshindi.
Mtoto Moureen Julius (12) akilia kwa furaha baada ya kuibuka mshindi.
Kilio cha furaha kwa Moureen Julius.
Wow.....!!!...Hongera Mwanangu.
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer, akikabidhi kitita cha Shilingi Milioni tano za Kitanzania kwa Supa Staa wa Shindano la "MO Kids Got Talent 2013" Moureen Julius (12). Wanaoshuhudia tukio hilo ni baba mzazi wa Moureen pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Frost Africa, Bw. Peter Sekasiko ambao ndio waandaji wa shindano hilo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Frost Africa, Bw. Peter Sekasiko, akiwa ameongozana na Supa Staa wa Shindano la "MO Kids Got Talent 2013" Moureen Julius (12) huku nyuma yao wakiwa na ulinzi mkali kuelekea kuzungumza na waandishi wa habari.
Supa Staa wa Shindano la "MO Kids Got Talent 2013" Moureen Julius (12), akifanya mahojiano na waandishi wa habari. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer.
Sehemu ya watoto, wazazi/walezi waliohudhuria fainali za shindano la "MO Kids Got Talent 2013" lililofanyika mwishoni mwa juma kwenye hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria hafla hiyo.