WAANDISHI WA HABARI WAANZA KUMSUSIA NAIBU WAZIRI WA HABARI JUMA NKAMIA


http://polis.parliament.go.tz/images/Pictures/1625.jpg NA KAROL VICENT
SIKU moja kupita Baada ya Rais Jakaya kikwete kuwapisha Baraza jipya la mawaziri, Naibu waziri mpya wa Habari na michezo Juma Nkamia ameonja Joto la Jiwe baada ya kususiwa na Waandishi wa habari wa vyombo vya watu Binafsi pamoja mashirika ya dini.

Taarifa ambazo Mwandishi wa mtandao huu amezipata kutoka ndani ya Wizara ya hiyo ya Habari zinasema tukio hilo lilitokea wakati, Naibu huyo alipokuwa anakabidhiwa ofisi za Wizara hiyo ili kuanza kazi,

Chanzo hicho kinasema, Chombo kimoja cha habari tu ndio kiliwepoa ambacho chombo kinatoka shirika la Utangazaji nchini TBC one,

Uchanguzi uliofanywa na Mwandishi wa mtandao huu unasema kitendo cha waandishi kususia mkutano huo ni kutokana na mazimo yaliyotolewa na Wamiliki wa Vyombo vya habari Nchini (MOAT) Kutoandika habari zozote zinazomuhusu Waziri wa habari Dkt. Fenella Mukangara pamoja na
Mkurugenzi wa Idara ya Habari maelezo kutokana na kufungiwa magazeti ya mtanzani pamoja Gazeti la Mwanachi,huwenda ikawasababu.

Vilevile Sababu nyingine iliyotajwa ni wakati mbunge huyo wa Kondoa kusini Wakati anachangia Bajeti ya Wizara ya Habari na Michezo kwa Mwaka 2013-2014 aliwaonyesha Dharau kwa Baraza la Habari nchini (MCT) kwa kusema Chombo hicho ni “ngios”na wala hakiko kwa ajiri ya kumsimamia waandishi wa habari nchini huwenda ikawa sababu.
 

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post